Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mizingile—Kwa Nini Huvutia Sana?
    Amkeni!—1999 | Desemba 22
    • Mizingile ya Jumuiya ya Wakristo

      Kati ya mizingile mingi yenye kutokeza katika majengo ya Jumuiya ya Wakristo, ulio mdogo zaidi ni ule wa karne ya 15 wenye umbo la duara uliotengenezwa kwa mbao na kutiwa nakshi, ulio kwenye paa ya St. Mary Redcliffe, kanisa lililoko Bristol, Uingereza. Limepakwa rangi ya dhahabu na nyeusi, na lina kipenyo cha sentimeta 20 tu. Mzingile mashuhuri zaidi unapatikana kwenye Kanisa Kuu la Chartres la Ufaransa. Ulijengwa mnamo mwaka wa 1235, kwa mawe ya rangi ya buluu na nyeupe, una kipenyo cha meta 10.

      Mizingile mikubwa ya sakafuni iliwekwa katika makanisa makuu mengine ya enzi za kati katika Ufaransa na Italia, kutia ndani yale yaliyoko Amiens, Bayeux, Orléans, Ravenna, na Toulouse. Ule mzingile ulioko Reims uliharibiwa miaka 200 iliyopita, na mzingile wa Kanisa Kuu la Mirepoix una Mchoro ulio katikati.

      Kichapo kimoja chaandika hivi kuhusu kuwepo kwa mizingile kwenye majengo yenye kutokeza ya kidini: “Mzingile wa wapagani ulianza kutumiwa na kanisa la Kikristo la enzi za kati na kubadilishwa ufae matumizi yake yenyewe kwa kutia ndani ufananisho wa Kikristo katika ubuni huo.” Hivyo, yaelekea mizingile ilitumiwa katika makanisa ya Jumuiya ya Wakristo ili kuwakilisha maisha ya Mkristo, kulingana na mithiolojia iliyoanzishwa na Wamisri wa kale.

      Mizingile ya kanisa ilitumiwa pia kuonyesha kwa matendo safari zilizofungwa na washiriki wa vita takatifu kuelekea Yerusalemu. Kufika katikati kulifananisha kufika Yerusalemu na kupata wokovu. Kwa waabudu fulani mzingile ulikuwa njia ya majuto ambayo ingekamilishwa kwa kutembea kwa magoti ili kupata msamaha wa dhambi au kwa kuitembea kupatana na desturi, jambo ambalo lingechukua mahali pa kwenda hija kwenye Bara Takatifu.

  • Mizingile—Kwa Nini Huvutia Sana?
    Amkeni!—1999 | Desemba 22
    • Je, unashangaa kwamba ijapokuwa mizingile ina chanzo cha kipagani, inashirikishwa na Jumuiya ya Wakristo? Je, Ukristo wa kweli unaweza kupatana na ushirikina wa kipagani?

      Je, Inapatana na Imani ya Kikristo?

      Hata ingawa historia ya mizingile ni yenye kuvutia sana, itikadi zinazohusiana nayo hazipatani na imani ya Kikristo. Hakuna mahali popote ambapo Biblia hufundisha kwamba nafsi ya binadamu imetenganishwa na mwili na kwamba inaendelea kuishi mtu anapokufa. Badala yake, Biblia hufundisha kwamba nafsi ya binadamu yaweza kufa. Inasema: “Nafsi inayofanya zambi, itakufa.”—Ezekieli 18:4, Zaire Swahili Bible.

      Neno la Mungu, Biblia lina nguvu na limelinganishwa na upanga, “upanga wa roho.” Wakristo hutumia silaha hiyo kwa ustadi ili kushinda kiumbe wa roho aliye halisi, mwenye nguvu zipitazo za binadamu, asiyeonekana pamoja na roho waovu wake, si Zimwi linalosimuliwa katika ngano. (Waefeso 6:12, 17) Tokeo ni kwamba, wana imani isiyoshindwa na tumaini hakika la wokovu. Imani hiyo itawasaidia wapite mwisho wa mfumo huu wa mambo hadi kwenye ulimwengu mpya wenye uadilifu—jambo ambalo itikadi katika mithiolojia haziwezi kufanya kamwe.—2 Petro 3:13.

  • Mizingile—Kwa Nini Huvutia Sana?
    Amkeni!—1999 | Desemba 22
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 24]

      Matumizi ya Jumuiya ya Wakristo ya Mzingile

      Hivi karibuni Makao ya Watawa yaliyoko Westminster, London, yalitokeza kitambaa kipya cha madhabahu kilichotiwa nakshi. Ona mzingile ulio katikati unaozungukwa na herufi “Α” (alpha, “MWANZO”) na “Ω” (omega, “MWISHO”). Katikati ya ubuni wa mzingile huu, ona “MIMI NIKO,” linalowakilisha Yehova, “MIMI NIKO” mkuu anayerejezewa kwenye Kutoka 3:14, King James Version. Huo ni mfano wa kisasa wenye kuvutia unaoonyesha uhusiano wa karibu kati ya mzingile na dini leo.

      [Hisani]

      Picha: David Johnson

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki