-
Je, Mungu Alikubali Biashara ya Watumwa?Amkeni!—2001 | Septemba 8
-
-
Utumwa na Wakristo
Wakristo wa karne ya kwanza waliishi chini ya mfumo wa uchumi wa Milki ya Roma ambao uliruhusu utumwa. Kwa hiyo, Wakristo fulani walikuwa watumwa na wengine walimiliki watumwa. (1 Wakorintho 7:21, 22) Lakini, je, hilo lilimaanisha kwamba wanafunzi wa Yesu walikandamiza watumwa wao? Hasha! Hata sheria ya Roma iwe iliruhusu nini, tunaweza kuwa na uhakika kwamba Wakristo hawakuwakandamiza wale waliokuwa chini ya mamlaka yao. Hata mtume Paulo alimhimiza Filemoni amtendee mtumwa wake Onesimo, aliyekuwa amekuwa Mkristo, kama “ndugu.”b—Filemoni 10-17.
-
-
Je, Mungu Alikubali Biashara ya Watumwa?Amkeni!—2001 | Septemba 8
-
-
b Baadhi ya Wakristo leo vilevile ni waajiri; wengine wameajiriwa kazi. Kama vile mwajiri Mkristo hawakandamizi wale wanaomfanyia kazi, wanafunzi wa Yesu katika karne ya kwanza waliwatendea watumishi wao kwa kupatana na kanuni za Kikristo.—Mathayo 7:12.
-