-
Sherehe Ambazo Zinamchukiza Mungu“Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
-
-
5. Kwa nini tunaweza kuwa na hakika kwamba Yesu hakuzaliwa Desemba 25?
5 Biblia haitaji popote maadhimisho ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Yesu. Kwa kweli, hata tarehe yenyewe ya kuzaliwa kwake haijulikani. Hata hivyo, tuna hakika kwamba hakuzaliwa Desemba 25, wakati ambapo kwa kawaida kunakuwa na baridi kali katika eneo alimozaliwa.b Sababu moja ni kwamba Luka aliandika kuwa Yesu alipozaliwa, “wachungaji [walikuwa] wakiishi nje,” wakichunga makundi yao. (Luka 2:8-11) Ikiwa wachungaji walikuwa “wakiishi nje” mwaka mzima, basi hakukuwa na haja ya kutaja jambo hilo. Hata hivyo, kwa kuwa Bethlehemu hupata mvua na theluji wakati wa majira ya baridi kali, makundi yalikuwa yakifungiwa ndani, nao wachungaji hawangekuwa “wakiishi nje.” Kwa kuongezea, Yosefu na Maria walienda Bethlehemu kwa kuwa Kaisari Augusto alikuwa ameagiza watu wahesabiwe. (Luka 2:1-7) Haielekei kwamba Kaisari angewaagiza watu ambao tayari walikuwa wakichukia utawala wa Roma, wasafiri kwenda majiji ya kwao kukiwa na baridi kali sana hivyo.
-
-
Sherehe Ambazo Zinamchukiza Mungu“Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
-
-
Vivyo hivyo, waabudu wa mungu Mithra walisherehekea “kuzaliwa kwa jua lisiloshindika” mnamo Desemba 25. “Krismasi ilianza wakati madhehebu ya jua yalipositawi nchini Roma,” karne tatu hivi baada ya kifo cha Kristo.—New Catholic Encyclopedia.
-