Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Chukua Msimamo Upande wa Ibada ya Kweli
    Biblia Inafundisha Nini Hasa?
    • KRISMASI ILIANZIA WAPI?

      9. Desemba 25 ilichaguliwaje kuwa siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu?

      9 Watu walitenga Desemba 25 kuwa siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu mamia ya miaka baada ya yeye kuishi duniani. Lakini Yesu hakuzaliwa siku hiyo, inaonekana alizaliwa mwezi wa Oktoba.a Basi, kwa nini Desemba 25 ilichaguliwa? Inaelekea kwamba baadaye watu fulani waliodai kuwa Wakristo “walitaka tarehe hiyo ipatane na sherehe ya kipagani ya Waroma ya ‘kuzaliwa kwa jua lisiloshindwa.’” (The New Encyclopædia Britannica) Wakati wa majira ya baridi kali, jua lilipoonekana kuwa hafifu zaidi, wapagani walifanya sherehe ili kulifanya jua lirudi na kuwaletea joto na nuru. Walidhani kwamba jua lilianza kurudi Desemba 25. Katika jitihada za kuwafanya wapagani wawe Wakristo, viongozi wa kidini waliikubali sherehe hiyo na kujaribu kuifanya ionekane kuwa ya “Kikristo.”b

  • Chukua Msimamo Upande wa Ibada ya Kweli
    Biblia Inafundisha Nini Hasa?
    • b Sherehe ya Saturnalia pia ilichangia kuchaguliwa kwa Desemba 25. Sherehe hiyo inayomheshimu mungu wa kilimo wa Waroma ilifanywa Desemba 17 hadi 24. Katika sherehe hiyo ya Saturnalia, watu walikula na kunywa, walijitumbuiza na kupeana zawadi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki