-
Kupiga Mbiu ya Kurudi kwa BwanaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Nelson H. Barbour, wa Rochester, New York, aliamini kwamba lengo la kurudi kwa Kristo si kuharibu familia za dunia bali kuzibariki na kwamba kuja kwake kungekuwa si katika mwili bali akiwa roho. Aa! hilo lilipatana na yale ambayo Russell na washirika wake katika Allegheny walikuwa wameamini kwa muda fulani!b Ingawa hivyo, ajabu ni kwamba Barbour aliamini kutokana na unabii mbalimbali unaohusu wakati wa Kibiblia kwamba Kristo alikuwa tayari yupo (bila kuonekana) na kwamba wakati ulikuwa umefika wa kufanya kazi ya mavuno ya kukusanya “ngano” (Wakristo wa kweli waliojumuika kuwa jamii ya Ufalme).—Mt., sura 13.
-
-
Kupiga Mbiu ya Kurudi kwa BwanaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
b Wala Barbour wala Russell sio waliokuwa wa kwanza kueleza kurudi kwa Bwana kuwa kuwapo kusikoonekana. Mapema zaidi, Sir Isaac Newton (1642-1727) alikuwa ameandika kwamba Kristo angerudi na kutawala “bila kuonekana kwa wanadamu.” Katika 1856, Joseph Seiss, mhudumu Mluther katika Philadelphia, Pennsylvania, alikuwa ameandika juu ya kuja kwa pili kwenye hatua mbili—pa·rou·siʹa, au kuwapo kusikoonekana, kukifuatwa na udhihirisho wenye kuonekana. Kisha, katika 1864, Benjamin Wilson alikuwa ametangaza Emphatic Diaglott yake ikiwa na usomekaji wa katikati ya mistari “kuwapo,” kwa ajili ya neno pa·rou·siʹa, si “kuja,” na B. W. Keith, mshirika wa Barbour, alikuwa ameelekeza uangalifu wa Barbour na washirika wake kwenye jambo hilo.
-