Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mizingile—Kwa Nini Huvutia Sana?
    Amkeni!—1999 | Desemba 22
    • Mzingile wa Krete

      Yaelekea mzingile ulioko Knossos, kwenye kisiwa cha Krete, ulijengwa miaka kadhaa baada ya ule wa Misri. Ijapokuwa mahali hapo hapajatambuliwa hasa, rekodi zaonyeshwa kwamba ulifanana na, lakini ni mdogo zaidi ya kiolezo cha Wamisri.a Neno la Kiingereza “labyrinth” labda lahusiana na neno laʹbrys, shoka lenye vichwa viwili vinavyowakilisha pembe mbili za fahali mtakatifu. Fahali huyo alikuwa mashuhuri katika ibada huko Minoa (ya Krete), iliyoathiriwa sana na mithiolojia.

      Mzingile wa Krete ulikuwa mashuhuri katika mithiolojia kwa sababu ya mkazi wake aliyeitwa Zimwi la Minos—mtu anayesimuliwa katika ngano mwenye kichwa cha fahali. Pasiphaë, mke wa Minos, mfalme wa Krete, kulingana na hekaya, alikuwa amezaa kiumbe hicho—hivyo kikapewa jina, Zimwi la Minos, linalomaanisha “Fahali wa Minos.” Kulingana na ngano hiyo, jiji la Athene lilishindwa vita na Krete, na watu wake walilazimishwa kutoa vijana 14 kila baada ya miaka tisa—wavulana 7 na wasichana 7—kuwa dhabihu kwa Zimwi la Minos. Vijana hao waliingizwa kwenye mzingile, ambapo walipotea kisha wakadhaniwa kuwa walinyafuliwa na Zimwi la Minos.

      Hata hivyo, baada ya muda, kijana mmoja, Theseus, alikubali mgawo huo na kuingia kwenye mzingile ili kuua dubwana hilo linalosimuliwa kwenye ngano. Inasemekana kwamba alipokutana nalo, Theseus aliliua Zimwi la Minos hilo kwa upanga wake. Ili kuponyoka, alirudi nyuma kwa kufuata uzi wa dhahabu, aliokuwa ameuweka chini kutoka kwenye mwingilio wa mzingile. Alikuwa amepewa uzi huo na Ariadne, binti ya Mfalme Minos.

      Michael Ayrton, aliyejenga muundo wa kukisia wa mzingile wa Wakrete, alieleza hivi: “Maisha ya kila mtu ni jambo lenye kutatanisha ambapo mwishowe hufikia kifo, hata baada ya kifo yawezekana kwamba hupita mzingile wa mwisho kabla ya kukoma kuwapo.” Katika maana hiyo, Theseus anayesimuliwa katika ngano alipoponyoka kutoka kwenye mzingile huo ulikuwa ufananisho wa kuzaliwa tena, alikwepa kifo. Tena, fundisho la hali ya kutokufa ya binadamu ni dhahiri.

      Ugiriki na Roma

      Kiolezo cha mzingile bora wa Wakrete huonekana kwenye sarafu zilizopatikana Knossos. Punde si punde kiolezo hicho kiliigwa na milki za Wagiriki na Waroma.

  • Mizingile—Kwa Nini Huvutia Sana?
    Amkeni!—1999 | Desemba 22
    • [Picha katika ukurasa wa 21]

      Sarafu za karne ya nne na ya tano K.W.K. zilizopatikana huko Knossos, Krete. Ona kiolezo cha mzingile na kichwa cha fahali, kinachowakilisha Zimwi la Minos

      [Hisani]

      Copyright British Museum

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki