Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jiji la Kale la Yerusalemu Liliharibiwa Mwaka Gani?—Sehemu ya Pili
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Novemba 1
    • ● Mabamba ya mambo ya kibiashara.

      Mabamba hayo ni nini? Mabamba mengi ya kipindi cha Milki Mpya ya Babiloni ni risiti zilizotambulika kisheria. Mabamba hayo yaliandikwa tarehe iliyoonyesha siku, mwezi, na mwaka wa mfalme aliyekuwa akitawala. Kwa mfano, bamba moja linasema kwamba ununuzi fulani ulifanywa “Nisani, tarehe 27, katika mwaka wa 11 wa Nebukadreza [ambaye pia aliitwa Nebukadneza wa Pili], mfalme wa Babiloni.”4

      Mfalme alipokufa au kuondolewa mamlakani na mfalme mpya kuanza kutawala, miezi iliyobaki katika mwaka wake wa utawala ilionwa kuwa mwaka wa kupokea mamlaka wa mfalme mpya.d5 Hiyo inamaanisha kwamba kuondoka kwa mtawala mmoja na mwingine kupokea mamlaka kulitokea mwaka uleule kwenye kalenda ya Wababiloni. Kwa hiyo, ni jambo linalopatana na akili kusema kwamba mabamba yaliyoonyesha mwaka ambao mfalme mpya alipokea mamlaka yanapaswa kuwa ya miezi iliyofuata mwezi wa mwisho wa mfalme aliyetangulia.

      Wataalamu wamesema nini? R. H. Sack alichunguza mabamba mengi ya mambo ya kibiashara ya kipindi cha Milki Mpya ya Babiloni. Katika mwaka wa 1972, Sack alichunguza mabamba mapya yanayopatikana katika Jumba la Makumbusho la Uingereza na ambayo hayajachapishwa na kuandika kwamba “yanavuruga kabisa” maoni ya awali kuhusu kipindi cha kuondoka mamlakani cha Nebukadneza wa Pili na kumpisha mwana wake Amel-Marduk (ambaye pia anaitwa Evil-merodach).6 Jinsi gani? Sack alijua mabamba yalionyesha kwamba Nebukadneza wa Pili alikuwa bado anatawala katika mwezi wa sita wa mwaka wake wa mwisho (mwaka wa 43). Lakini uchunguzi wa mabamba hayo mapya kuhusu mwaka ambao mfalme aliyefuata, Amel-Marduk, alipokea mamlaka, umeonyesha kwamba mabamba hayo ni ya mwezi wa nne na wa tano wa mwaka ambao ulifikiriwa kuwa mwaka wa mwisho wa Nebukadneza wa Pili.7 Bila shaka, miezi hiyo haipatani.

      Maandishi hayo yanaonyesha nini? Yanaonyesha kwamba muda uliopita baada ya mfalme mmoja kuondoka na mwingine kupokea mamlaka, haupatani. Kwa mfano, hati moja inaonyesha kwamba Nebukadneza wa Pili alikuwa bado anatawala katika mwezi wake wa kumi—miezi sita baada ya kipindi ambacho inawaziwa mtawala aliyepokea mamlaka baada yake alikuwa ameanza kutawala.8 Pia, kuna kutopatana kuhusiana na muda uliopita baada ya kuondoka kwa Amel-Marduk na kupokea mamlaka kwa Neriglisa, mtawala aliyefuata.9

      Kwa nini kutopatana huko ni muhimu? Kama ilivyotajwa awali, mapengo katika maandishi ya mfuatano wa matukio kuhusu Babiloni yanaonyesha kwamba huenda hakuna rekodi kamili ya mfuatano wa matukio hayo.10 Je, huenda kuna wafalme wengine wasiotajwa ambao walitawala katika vipindi hivyo vya kuondoka na kupokea mamlaka kwa wafalme? Ikiwa ndivyo, miaka kadhaa inapaswa kuongezwa kwenye kipindi cha Milki Mpya ya Babiloni. Kwa hiyo, maandishi ya mfuatano wa matukio kuhusu Babiloni na mabamba ya mambo ya kibiashara hayawezi kutumiwa kama msingi hakika wa kuthibitisha kwamba jiji la Yerusalemu liliharibiwa mwaka wa 587 K.W.K.e

  • Jiji la Kale la Yerusalemu Liliharibiwa Mwaka Gani?—Sehemu ya Pili
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Novemba 1
    • e Kuna mabamba ya mambo ya kibiashara kuhusu kipindi chote cha watawala wa Milki Mpya ya Babiloni. Miaka ya utawala wa wafalme hao inapojumlishwa na kuihesabu kurudi nyuma, kuanzia wakati wa Nabonido, mtawala wa mwisho wa Milki Mpya ya Babiloni, inaonekana kwamba jiji la Yerusalemu liliharibiwa mwaka wa 587 K.W.K. Hata hivyo, njia hiyo ya kuhesabu inaweza tu kuwa sahihi ikiwa kila mfalme alianza kutawala mwaka uleule ambao mfalme aliyemtangulia aliondoka, bila kipindi fulani kupita kati ya watawala hao.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki