-
Walikabiliana na Miiba Katika Miili YaoMnara wa Mlinzi—2002 | Februari 15
-
-
11. Siba alidai nini kuhusu Mefiboshethi, na tunajuaje kwamba dai lake lilikuwa la uwongo? (Ona kielezi-chini.)
11 Baadaye Mefiboshethi alilazimika kupambana na mwiba mwingine katika mwili wake. Mtumishi wake Siba alimchongea mbele ya Mfalme Daudi, ambaye alikuwa akikimbia Yerusalemu kwa sababu ya uasi wa Absalomu, mwana wa Daudi. Siba alisema kwamba Mefiboshethi si mwaminifu na alikuwa amebaki Yerusalemu akitumaini kujitwalia utawala.a Daudi aliamini uchongezi wa Siba na kumpa mwongo huyo shamba lote la Mefiboshethi!—2 Samweli 16:1-4.
-
-
Walikabiliana na Miiba Katika Miili YaoMnara wa Mlinzi—2002 | Februari 15
-
-
a Haielekei kwamba mtu aliyekuwa mwenye shukrani na mnyenyekevu kama Mefiboshethi angepanga njama kama hiyo kwa kujitakia makuu. Inaelekea alijua sifa ya uaminifu ya babake Yonathani. Ingawa alikuwa mtoto wa Mfalme Sauli, Yonathani alitambua kwa unyenyekevu kwamba Daudi alikuwa amechaguliwa na Yehova kuwa mfalme wa Israeli. (1 Samweli 20:12-17) Yonathani hangemfunza mwanawe mchanga kutamani mamlaka ya kifalme kwa kuwa alikuwa mzazi aliyemhofu Mungu na rafiki mwaminifu-mshikamanifu wa Daudi.
-