Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhuisha Mashahidi Wawili
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Na wale wa vikundi vya watu na makabila na ndimi na mataifa watatazama maiti zao kwa siku tatu na nusu, na wao hawaruhusu maiti zao zilazwe katika kaburi.

  • Kuhuisha Mashahidi Wawili
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Ufunuo 11:7-

  • Kuhuisha Mashahidi Wawili
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 21. (a) Wale maadui wa kidini wa mashahidi wawili walitumiaje kwa faida yao hali ya vita? (b) Uhakika wa kwamba zile maiti za mashahidi wawili ziliachwa bila kuzikwa ulionyesha nini? (c) Kipindi cha wakati cha siku tatu na nusu chapasa kionweje? (Ona kielezi cha chini.)

      21 Kutoka 1914 kufika 1918 mataifa yalikuwa yakishughulika na vita ya kwanza ya ulimwengu. Hisi za utukuzaji wa taifa zilipanda juu, na katika masika ya 1918, maadui wa kidini wa mashahidi wawili walijifaidi na hali hiyo. Walitumia kwa hila chombo cha Serikali cha kisheria hivi kwamba wahudumu wenye madaraka miongoni mwa Wanafunzi wa Biblia walitiwa gerezani kwa mashtaka bandia ya kufitini serikali. Wafanya kazi wenzi waaminifu waliduwaa. Utendaji wa Ufalme karibu ulikoma. Ilikuwa kana kwamba ile kazi ya kuhubiri ilikuwa imekufa. Katika nyakati za Biblia ulikuwa utovu wa heshima mbaya sana kutolazwa katika kaburi la ukumbusho. (Zaburi 79:1-3; 1 Wafalme 13:21, 22) Kwa hiyo, suto kubwa lingeshikamana na kuacha mashahidi wawili bila kuzikwa. Katika hewa yenye joto ya Palestina, maiti ikiwa peupe katika barabara wazi ingeanza kuvunda kikweli baada ya siku tatu na nusu halisi.c (Linga Yohana 11:39.) Elezo hili lenye mambo mengi katika unabii huonyesha aibu ambayo hao mashahidi wawili walilazimika kuvumilia. Hao ambao wametajwa hapo juu ambao walitiwa gerezani hata walikatazwa dhamana wakati kesi zao zilipokuwa kwenye rufani. Walifichuliwa peupe muda mrefu kutosha kuwa uvundo kwa wakazi wa “jiji kubwa.”

  • Kuhuisha Mashahidi Wawili
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Na baada ya siku tatu na nusu roho ya uhai kutoka kwa Mungu iliingia ndani yao, na wao wakasimama kwa nyayo zao, na hofu kubwa ikaanguka juu ya wale waliokuwa wakiona wao. Na wao wakasikia sauti kubwa kutoka mbingu ikisema kwao: ‘Njooni juu huku.’ Na wao wakaenda juu ndani ya mbingu kwa wingu na maadui wao wakaona wao.” (Ufunuo 11:11, 12, NW) Hivyo, wao walikuwa na ono kama lile la mifupa mikavu katika bonde ambalo Ezekieli alitembelea katika njozi. Yehova alipuliza juu ya hiyo mifupa mikavu, nayo ikawa hai, ikiandaa picha ya uzawa mpya wa taifa la Israeli baada ya miaka 70 ya utekwa katika Babuloni. (Ezekieli 37:1-14) Unabii huo muwili, katika Ezekieli na katika Ufunuo, ulikuwa na utimizo wao wa ki-siku-hizi wenye kutazamisha katika 1919, wakati Yehova aliporudisha mashahidi wake ‘waliokufa’ kwenye uhai wenye kusisimua.

  • Kuhuisha Mashahidi Wawili
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • c Angalia kwamba katika kuchunguza yanayopata maono ya watu wa Mungu wakati huu, inaonekana kwamba ingawa miezi 42 huwakilisha miaka mitatu na nusu halisi, siku tatu na nusu haziwakilishi kipindi halisi chenye saa 84. Inaelekea kwamba, kipindi mahususi cha siku tatu na nusu kimetajwa mara mbili (katika mstari wa 9 na 11) kukazia kwamba kingekuwa kipindi kifupi tu kikilinganishwa na miaka mitatu na nusu ya utendaji inayokitangulia.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki