-
Kuhuisha Mashahidi WawiliUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na wakati wao wamekwisha kumaliza kushuhudu kwao, hayawani-mwitu ambaye hupanda kutoka katika abiso atafanya vita na wao na kushinda wao na kuua wao. Na maiti zao zitakuwa katika njia pana ya jiji kubwa ambalo kwa maana ya kiroho huitwa Sodoma na Misri, ambako pia Bwana yao alitundikwa kwenye nguzo. Na wale wa vikundi vya watu na makabila na ndimi na mataifa watatazama maiti zao kwa siku tatu na nusu, na wao hawaruhusu maiti zao zilazwe katika kaburi. Na wale wanaokaa juu ya dunia hushangilia juu yao na kujifurahisha wenyewe, na wao watapelekeana zawadi, kwa sababu manabii wawili hawa walitesa wale wanaokaa juu ya dunia.”—Ufunuo 11:7-10, NW.
-
-
Kuhuisha Mashahidi WawiliUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
21. (a) Wale maadui wa kidini wa mashahidi wawili walitumiaje kwa faida yao hali ya vita? (b) Uhakika wa kwamba zile maiti za mashahidi wawili ziliachwa bila kuzikwa ulionyesha nini? (c) Kipindi cha wakati cha siku tatu na nusu chapasa kionweje? (Ona kielezi cha chini.)
21 Kutoka 1914 kufika 1918 mataifa yalikuwa yakishughulika na vita ya kwanza ya ulimwengu. Hisi za utukuzaji wa taifa zilipanda juu, na katika masika ya 1918, maadui wa kidini wa mashahidi wawili walijifaidi na hali hiyo. Walitumia kwa hila chombo cha Serikali cha kisheria hivi kwamba wahudumu wenye madaraka miongoni mwa Wanafunzi wa Biblia walitiwa gerezani kwa mashtaka bandia ya kufitini serikali. Wafanya kazi wenzi waaminifu waliduwaa. Utendaji wa Ufalme karibu ulikoma. Ilikuwa kana kwamba ile kazi ya kuhubiri ilikuwa imekufa. Katika nyakati za Biblia ulikuwa utovu wa heshima mbaya sana kutolazwa katika kaburi la ukumbusho. (Zaburi 79:1-3; 1 Wafalme 13:21, 22) Kwa hiyo, suto kubwa lingeshikamana na kuacha mashahidi wawili bila kuzikwa. Katika hewa yenye joto ya Palestina, maiti ikiwa peupe katika barabara wazi ingeanza kuvunda kikweli baada ya siku tatu na nusu halisi.c (Linga Yohana 11:39.) Elezo hili lenye mambo mengi katika unabii huonyesha aibu ambayo hao mashahidi wawili walilazimika kuvumilia. Hao ambao wametajwa hapo juu ambao walitiwa gerezani hata walikatazwa dhamana wakati kesi zao zilipokuwa kwenye rufani. Walifichuliwa peupe muda mrefu kutosha kuwa uvundo kwa wakazi wa “jiji kubwa.”
-