Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 2/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nini Siri ya Furaha?
  • DNA na Hati-Kunjo za Bahari Iliyokufa
  • Kuzorota kwa Familia Kulikoenea Sana
  • Dhambi za Akina Baba
  • Kinachokaribia Kutokea: Nchi ya Kwanza ya Asia Isiyo na Misitu
  • “Wabarikiwa Ni Mashahidi wa Yehova”
  • Mrembeshaji kwa Ajili ya Tembo
  • Majeruhi Wachanga wa Vita
  • Peni Lenye Thamani Ndogo
  • Tumaini kwa Wenye Kushikwa na Ugonjwa wa Moyo
  • Akina Baba Sababu Inayofanya Watoweke
    Amkeni!—2000
  • Idadi ya Familia za Mzazi Mmoja Inaongezeka
    Amkeni!—2002
  • Ukweli Kuhusu Hati-Kunjo za Bahari ya Chumvi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Tembo—Marafiki au Maadui?
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 2/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Ni Nini Siri ya Furaha?

Ingawa Waingereza ni wenye afya zaidi na matajiri zaidi kuliko walivyokuwa miaka 25 iliyopita, kwa ujumla hawana furaha sana, kulingana na uchunguzi ulioripotiwa katika The Daily Telegraph la London. Mtaalamu mmoja Mmarekani wa elimu ya jamii, akikubaliana na matokeo haya ya Ripoti ya Tabia za Jamii kutoka Ofisi Kuu ya Takwimu, asisitiza kwamba furaha ya kweli huja kutokana na kuwa na “maana katika maisha” kutia ndani “mfuatio wa miradi inayostahili.” Baada ya kuhoji karibu watu 400, watafiti wawili wa New Zealand walifikia mkataa sawa na huo—kwamba watu wengi huona furaha kuwa inatokana na “utambuzi wa utaratibu na kusudi katika kuwapo kwao.” Watu waliofunga ndoa na wale wenye usadikisho wenye nguvu wa kidini huelekea kupata uradhi zaidi. Likifikiria kudidimia kwa ndoa na imani za kidini katika Uingereza, gazeti hilo la habari lilimalizia kwamba “tukiwa taifa, tutaendelea kukosa furaha zaidi.”

DNA na Hati-Kunjo za Bahari Iliyokufa

Kufasiri Hati-kunjo za kale za Bahari Iliyokufa kulianza muda mfupi baada ya ugunduzi wazo katika jangwa la Yudea katika 1947. Kufikia wakati huu, hati-kunjo 15 hivi zimetafsiriwa. Zilizobaki ni vipande vipatavyo 10,000 vyenye ukubwa wa ukucha wa kidole-gumba zilizotokana na mamia ya hati-kunjo nyinginezo. Kuunganisha hivyo vipande kumefadhaisha sana. Kingo zimechakaa mno kuweza kuingiana pamoja kama fumbo la kuunganisha vipande vya kufanyiza picha, na kwa kuwa kila kipande kina herufi chache tu, haviwezi kuunganishwa kwa kutumia maana. Sasa, kulingana na International Herald Tribune, ufundi wa kisayansi utasaidia. Jinsi gani? Maandishi yalifanywa kwenye ngozi za wanyama, kwa hiyo upambanuzi wa kutumia DNA waweza kutambulisha spishi, aina, na mnyama yule ambaye kila kipande kinatoka. Wasomi wanatumaini kwamba jambo hili litafanya iwe rahisi zaidi kupanga na kupatanisha hivyo vipande.

Kuzorota kwa Familia Kulikoenea Sana

“Kotekote ulimwenguni, katika nchi tajiri na vilevile nchi maskini, muundo wa maisha ya familia unapitia mabadiliko makubwa mno,” lataarifu The New York Times, likieleza juu ya ripoti fulani ya majuzi. “Misukosuko katika familia haipati tu watu wa kikundi kimoja cha kijamii au nchi.” Hiyo ripoti, inayotegemea uchunguzi wa nchi nyingi uliofanywa na Baraza la Idadi ya Watu, hutaja mielekeo kama vile kuongezeka kwa talaka na kuongezeka kwa idadi ya akina mama wasioolewa. “Lile wazo la kwamba familia ni mfanyizo wenye uthabiti na ulioshikamana ambao katika huo baba hutumikia akiwa mwandalizi wa kiuchumi naye mama hutumikia akiwa mpaji wa utunzi wa kihisia-moyo ni ngano,” asema Judith Bruce, mmoja wa waanzilishi wa huo uchunguzi. Kuvunjika kwa ndoa, ama kwa kutengana, kuachwa bila msaada, au talaka, kunaongezeka kwa haraka mno, na akina mama wasioolewa wamejaa karibu kila mahali. Kwa kielelezo, uzaaji mwingi mno kufikia thuluthi ya uzaaji wote katika Ulaya Kaskazini ni wa akina mama wasioolewa. Watafiti wanataja “kuwekwa huru kwa wanawake,” kutia ndani hali yao ya kiuchumi na daraka linaloongezeka kazini, kuwa kisababishi kikuu kwa mabadiliko mengi katika familia. Tofauti iliyo wazi kwa mwelekeo huo ni Japani, ambako akina mama wasioolewa na nyumba za mzazi mmoja bado ni chache sana kwa kulinganisha. Hata hivyo, robo tatu ya akina baba waliotaliki huko hawalipi utegemezo wa watoto.

Dhambi za Akina Baba

Wizara ya Mambo ya Kidini ya Israeli imekubali kwamba hiyo huweka orodha ya watu wastahilio adhabu ya maelfu kadhaa ya Wayahudi ambao wakatazwa kuoa Wayahudi wengine kwa sababu ya kuwa wazao wa mahusiano yaliyokatazwa. Wenzi wapangao kufunga ndoa hudai kwamba wao huja kutambua hilo wakati mipango yao ya arusi ikaribiapo kumalizika. Baraza la marabi Waothodoksi ndilo lenye kufanya uamuzi wa mwisho. Wakati Shoshana Hadad na Masoud Cohen walipojaribu kusajili mwana wao mwenye umri wa miaka minne kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani, walipata kwamba ndoa yao ya 1982 ilikuwa imeharamishwa “kwa sababu ya dhambi iliyofanywa na familia ya mke miaka ipatayo 2,500 iliyopita,” laripoti Times Union la Albany, New York. Hilo laongeza hivi: “Hukumu hiyo yategemea uvumi wa kihistoria. Marabi wanaamini kwamba mzazi wa kale sana wa Hadad . . . alifunga ndoa isivyo halali na mtalikiwa katika mwaka 580 hivi K.W.K.” Tangu wakati huo, hakuna yeyote katika familia ya Hadad ameruhusiwa kufunga ndoa na yeyote aitwaye Cohen. Wacohen huonwa kuwa wazao wa makuhani awali wa hekalu na ni lazima wafuate makatazo ya kipekee. “Ikiwa babu wa kale mno alifanya jambo katika siku za Hekalu la Sulemani, je, ni lazima tuteseke kwa ajili yalo hadi siku hii?” akauliza Shoshana. Wizara ya Mambo ya Kidini yasema kwamba mume na mke hao wanaweza kukabili mashtaka ya jinai eti kwa kupotosha rabi aliyewafungisha ndoa.

Kinachokaribia Kutokea: Nchi ya Kwanza ya Asia Isiyo na Misitu

Filipino yakabili kukatwa kabisa kwa misitu, laonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP). “Misongo ya idadi ya watu na mazoea yasiyozuiliwa ya kukata miti” yanaharibu zaidi na zaidi bara lililofunikwa na miti katika Filipino. Kabla ya vita ya ulimwengu ya pili, asilimia 60 hadi 70 ya hiyo nchi ilikuwa imefunikwa na misitu. Leo, ni asilimia 15 tu imefunikwa. “Kufikia mwaka 2000,” laripoti Update, jarida la UNDP, “Filipino huenda ikawa nchi ya kwanza ya Asia kupoteza bara layo lote lililo msitu na lililofunikwa kwa miti.”

“Wabarikiwa Ni Mashahidi wa Yehova”

Kama ilivyo katika nchi nyinginezo nyingi, kashfa ya damu imezuka katika Italia. Inadaiwa kwamba maelfu ya lita za damu yalisambazwa kwa vitovu vya utiaji-damu mishipani bila ya kuchunguzwa vya kutosha au bila hatua zifaazo za usalama kuchukuliwa, hivyo zikihatarisha maelfu ya watu kwa maambukizo ya magonjwa kama vile UKIMWI na mchochota wa ini. Akitoa maelezo kuhusu hali hiyo yenye kushtua ambayo iliweka faida juu ya afya ya kibinafsi, Luigi Pintor, mhariri wa gazeti la habari la Italia Il Manifesto, alianza makala yake kwa maneno haya: “Wabarikiwa ni Mashahidi wa Yehova, ambao . . . hukataa utiaji-damu mishipani kwa sababu za kidini. Wasomapo magazeti ya habari siku hizi, ni wao pekee ambao hawatakuwa na wasiwasi kuhusu kile kinachoendelea . . . katika biashara za damu na kliniki ziuzazo na kuweka damu, umajimaji wa damu, na vifanyizo vinavyohusiana na hivyo kwa watu wenzao.”

Mrembeshaji kwa Ajili ya Tembo

Tembo katika jimbo la kusini mwa India la Kerala hubeba mizigo mizito, mara nyingi kwenye pembe zao ndefu. Lakini wengi wa tembo hao pia hutumiwa katika misafara ya hekalu na kwenye sherehe za kidini. Kabla ya pindi hizi, mrembeshaji mtaalamu huwafanyia, si mfanyizo mpya, bali upunguzaji wa pembe zao. Mtu pekee katika Kerala anayefanya kazi hii ya kujisulubu, P. K. Sasidharan, alipata stadi zake kutoka kwa babu yake. Yeye huamuaje ni kiwango gani cha kupunguza? Habari halisi ya kazi—ikitegemea kimo, ukubwa, na umbo la mwili wa tembo—ni siri ya familia iliyolindwa vyema. Huyo mnyama akiwa mwenye ushirikiano, kazi hiyo huchukua muda wa saa tatu hivi, lakini tembo mwenye kusumbua hutokeza hatari na wakati mrefu zaidi ungehitajiwa. Kando na sababu za kiurembo, pembe za tembo wafanyao kazi huhitaji kupunguzwa baada ya kila miaka miwili ili kudumisha urefu ufaao kubeba mizigo.

Majeruhi Wachanga wa Vita

Wakati mmoja, majeruhi wa vita sanasana walikuwa wanajeshi. Sivyo ilivyo tena. Katika miaka kumi iliyopita, vita vimelemaza na kuua watoto wengi zaidi ya wanajeshi. Watoto milioni mbili hivi wamekufa katika vita kwa mwongo uliopita, yasema The State of the World’s Children 1995, ripoti iliyotolewa na Hazina ya Watoto ya Umoja wa Mataifa. Watoto milioni 4 hadi 5 zaidi wamekatwa viungo, zaidi ya milioni 5 kulazimika kukaa katika kambi za wakimbizi, na zaidi ya milioni 12 huachwa bila makao. Ripoti hiyo yataarifu hivi: “Hizi ni tarakimu za aibu. Nazo hutokeza huzuni kwa vizazi vya wakati ujao na mng’ang’ano wao wa kupata uthabiti na muungano wa kijamii.”

Peni Lenye Thamani Ndogo

“Siku hizi watu wengi hawawezi hata kusimama ili kuokota peni,” akasema msemaji wa Britain’s Royal Mint. Lakini si katika Uingereza pekee. Katika Marekani, mapeni mengi mno hupotezwa au kutupwa kila siku hivi kwamba banki zinapata upungufu. Hivi majuzi, Key Bank ya New York ilitoa senti 55 kwa mtu yeyote ambaye alileta mapeni 50. Likiwa tokeo, sarafu milioni tano zilikusanywa kwa majuma mawili. Katika Massachusetts kitovu kimoja cha kutia taka dawa hukusanya dola 1,000 kila siku zikiwa pesa ndogo-ndogo—nyingi zikiwa peni—kwa kuchekecha majivu, laripoti The Sunday Times la London.

Tumaini kwa Wenye Kushikwa na Ugonjwa wa Moyo

“Mbeleni ilifikiriwa kwamba mfuatano kuelekea kukosa kufanya kazi kwa moyo kulikuwa kusikoepukika baada ya jeraha baya sana la moyo, lakini kuepusha uharibifu huo kwawezekana kwa kufanya mazoezi,” adai Dakt. Peter Liu, mkurugenzi wa utafiti wa moyo kwenye Hospitali ya Toronto. Kufuatia uchunguzi wenye mataraja mazuri waliofanyiwa panya, Cardiac Function Clinic ya hiyo hospitali iliwafanya wagonjwa wa moyo “watembee kwa umbali wenye kuongezeka hatua kwa hatua kila siku,” laripoti The Globe and Mail. “Matokeo ya mwanzoni yaonyesha kwamba kutembea kwa angalau kilometa moja kila siku kwaweza kuepusha ‘mkondo wenye kuwa mbaya’ wa moyo kushindwa kufanya kazi katika binadamu vilevile.” Hata hivyo, huo mwendo wapasa kuwa wenye bidii kwa kiasi, na kutembea kufanywe chini ya usimamizi, akasema Dakt. Liu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki