Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kulea Mtoto Aliye na Down Syndrome—Kazi Ngumu Inayothawabisha
    Amkeni!—2011 | Juni
    • Down syndrome (DS) ni nini?a Kwa ufupi, DS ni kasoro katika chembe za urithi ambayo hutokea katika mtoto 1 kati ya 730 huko Marekani.b Watoto walio na DS wana viwango mbalimbali vya tatizo la kujifunza na kuzungumza na pia wana tatizo la kudhibiti misuli yao. Pia wanachukua muda kukomaa kihisia, kiakili, na katika mahusiano yao na wengine.

      Tatizo hilo huathiri uwezo wa kujifunza wa mtoto kwa kadiri gani? Jason, ambaye ana DS, anaeleza hivi katika kitabu alichoshiriki kuandika Count Us In—Growing Up With Down Syndrome: “Sidhani ni ulemavu. Ni tatizo la kujifunza kwa sababu unajifunza polepole. Si tatizo baya sana.” Hata hivyo, kila mtoto aliye na DS ni tofauti na ana vipawa vyake. Kwa kweli, baadhi yao wanaweza kujifunza vya kutosha kufaidi jamii na kuwa na maisha yenye kuridhisha.

      Hakuna chochote kinachoweza kufanywa ili kuzuia tatizo hilo la chembe za urithi, iwe ni kabla au wakati wa uja-uzito. Hakuna yeyote anayepaswa kulaumiwa.

  • Kulea Mtoto Aliye na Down Syndrome—Kazi Ngumu Inayothawabisha
    Amkeni!—2011 | Juni
    • b Jina hilo lilitokana na John Langdon Down, daktari Mwingereza ambaye ndiye aliyekuwa wa kwanza kufafanua kwa usahihi tatizo hilo mnamo 1866. Katika mwaka wa 1959, Mfaransa Jérôme Lejeune, ambaye ni mtaalamu wa chembe za urithi aligundua kwamba watoto wenye DS huzaliwa wakiwa na kromosomu ya ziada katika chembe zao, hivyo wanakuwa na jumla ya kromosomu 47 badala ya 46. Baadaye watafiti waligundua kwamba kromosomu hiyo ya ziada ilikuwa nakala ya kromosomu ya 21.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki