Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Musa—Mtu Halisi au wa Hadithi?
    Amkeni!—2004 | Aprili 8
    • Musa anaondoka Midiani na kumwendea Farao, akitaka awaachilie watu wa Mungu. Mtawala huyo mkaidi anapokataa, nchi ya Misri inakumbwa na mapigo kumi makali. Pigo la kumi linawaua wazaliwa wa kwanza wa Misri, na Farao mwenye huzuni anawaachilia Waisraeli.—Kutoka, sura ya 5-13.

      Watu wengi wanayajua matukio hayo. Lakini je, ni matukio ya kweli? Wengine wanadai kwamba kwa kuwa jina la Farao huyo halijatajwa, basi simulizi hilo si la kweli.e Hata hivyo, Hoffmeier, aliyenukuliwa awali, anasema kwamba mara nyingi waandishi Wamisri hawakuyataja majina ya adui za Farao kimakusudi. Anasema: “Wanahistoria hawawezi kusema kwamba Mfalme Thutmose wa 3 hakupigana huko Megido eti kwa sababu majina ya wafalme wa Kadeshi na Megido hayakutajwa.” Hoffmeier anasema kwamba Farao huyo hakutajwa “kwa sababu nzuri za kidini.” Sababu moja ni kwamba kwa kutotaja jina la Farao huyo, simulizi hilo linaelekeza uangalifu kwa Mungu, wala si kwa Farao.

  • Musa—Mtu Halisi au wa Hadithi?
    Amkeni!—2004 | Aprili 8
    • e Wanahistoria fulani wanasema kwamba Farao aliyetawala wakati Waisraeli walipotoka Misri ni Thutmose wa 3. Wengine wanasema alikuwa Amenhotep wa 2, Ramses wa 2, na kadhalika. Kwa sababu ya mvurugo wa rekodi za ukoo za Misri, ni vigumu kujua kwa hakika jina la Farao huyo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki