Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yesu ‘Aimarisha Haki Duniani’
    Mkaribie Yehova
    • 16, 17. (a) Yesu alionyeshaje haki alipohubiri habari njema za Ufalme wa Mungu? (b) Yesu alionyeshaje kwamba haki yake ilikuwa yenye rehema?

      16 Pili, Yesu alionyesha haki alipohubiri habari njema za Ufalme wa Mungu. Hakuwa na ubaguzi. Badala yake, alijitahidi sana kuwahubiria watu wa kila aina, matajiri kwa maskini. Tofauti na Yesu, Mafarisayo waliwapuuza watu maskini wa kawaida na kuwaita kwa madharau ʽam-ha·ʼaʹrets, yaani, “watu wa ardhi.” Kwa ujasiri, Yesu alipinga ukosefu huo wa haki. Alipowafundisha watu habari njema, alipokula nao, alipowalisha, alipowaponya, au hata kuwafufua, aliunga mkono haki ya Mungu ambaye anataka “watu wa namna zote” waokolewe.c—1 Timotheo 2:4.

      17 Tatu, Yesu alionyesha haki yenye rehema nyingi. Alijitahidi sana kuwasaidia watenda-dhambi. (Mathayo 9:11-13) Alikuwa tayari kuwasaidia watu ambao hawangeweza kujilinda. Kwa mfano, Yesu hakuwa kama viongozi wa kidini ambao waliwashuku watu wote wasio Wayahudi. Aliwasaidia na kuwafundisha baadhi yao kwa rehema, hata ingawa alitumwa hasa kwa Wayahudi. Alikubali kumponya kimuujiza mtumishi wa ofisa mmoja wa jeshi la Roma, na kusema: “Kwa yeyote katika Israeli sijapata imani kubwa sana kadiri hii.”—Mathayo 8:5-13.

      18, 19. (a) Yesu aliwaheshimu wanawake kwa njia gani? (b) Mfano wa Yesu unatusaidiaje kuona uhusiano uliopo kati ya ujasiri na haki?

      18 Vilevile, Yesu hakuunga mkono maoni yaliyoenea kuhusu wanawake. Badala yake, alitenda yaliyo haki kwa ujasiri. Wanawake Wasamaria walionwa kuwa wachafu kama watu wasio Wayahudi. Hata hivyo, Yesu hakusita kumhubiria yule mwanamke Msamaria penye kisima cha Sikari. Kwa kweli, Yesu alijitambulisha waziwazi kwa mara ya kwanza kuwa Mesiya aliyeahidiwa alipoongea na mwanamke huyo. (Yohana 4:6, 25, 26) Mafarisayo walisema kwamba wanawake hawakupaswa kufundishwa Sheria ya Mungu, lakini Yesu alitumia wakati mwingi na nguvu kuwafundisha wanawake. (Luka 10:38-42) Na ingawa mapokeo yalisema kwamba wanawake hawawezi kutoa ushahidi unaoaminika, Yesu aliwaheshimu wanawake kadhaa kwa kuwapa nafasi ya pekee ya kuwa watu wa kwanza kumwona baada ya kufufuliwa. Hata aliwaambia wawapashe wanafunzi wake wanaume habari za tukio hilo muhimu sana!—Mathayo 28:1-10.

  • Yesu ‘Aimarisha Haki Duniani’
    Mkaribie Yehova
    • 20, 21. Katika siku zetu, Mfalme wa Kimesiya ametekelezaje haki duniani pote na katika kutaniko la Kikristo?

      20 Tangu alipowekwa kuwa Mfalme wa Kimesiya mwaka wa 1914, Yesu ametekeleza haki duniani. Jinsi gani? Amekuwa na jukumu la kuhakikisha kwamba unabii aliotoa kwenye Mathayo 24:14 unatimizwa. Wafuasi wa Yesu duniani wamewafundisha watu wa nchi zote ukweli kuhusu Ufalme wa Yehova. Kama Yesu, wamehubiri bila ubaguzi na kwa njia ya haki, wakijitahidi kumpa kila mtu—mtoto kwa mzee, tajiri kwa maskini, wanaume kwa wanawake—nafasi ya kumjua Yehova, Mungu wa haki.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki