Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yucca Usio na Miiba—Mmea Wenye Kubadilika Isivyo Kawaida
    Amkeni!—1998 | Januari 22
    • UNAFANANA na mitishamba, unafanana na sabuni, ni mtamu na wenye lishe. Mmea huu usio wa kawaida una sifa hizi zote bainifu, na nyingine nyingi! Unajulikana vizuri na Waamerika wa Kati lakini si kwa jina yucca usio na miiba. Ikiwa ungetumia neno hilo katika Amerika ya Kati, watu wengi zaidi wangeelekea kuitikia kwa upole na kukukodolea macho yenye udadisi. Hata hivyo, tabasamu pana ya utambuzi ingeonekana mara moja ikiwa ungetaja itabo, izote, au daguillo, kama mmea huo ujulikanavyo kikawaida katika Kosta Rika, Guatemala, Honduras, na Nikaragua. Watu wa Kosta Rika na Waamerika wengine wa Kati hufurahia ladha ya maua yake katika vyakula vya namna nyingi.

  • Yucca Usio na Miiba—Mmea Wenye Kubadilika Isivyo Kawaida
    Amkeni!—1998 | Januari 22
    • Wakati wa msimu wa kiangazi katika Kosta Rika, hasa miezi ya Februari na Machi, mamia ya maua ya rangi ya pembe ya ndovu, yenye umbo la kengele, huvika taji mmea wa itabo. Inaonekana kuwa mahali pote kwa wakati uleule kwa kuwa inauzwa mahali pa soko na wachuuzi wa barabarani! Kwa kutofautisha kabisa na majani magumu, yenye umbo la singe, maua haya mororo huchanua katika kishada yakikua barabara katikati ya mmea, na yakiwa wima.

  • Yucca Usio na Miiba—Mmea Wenye Kubadilika Isivyo Kawaida
    Amkeni!—1998 | Januari 22
    • Ni Mtamu kwa Kulika

      Frances Perry, mtungaji wa Flowers of the World, aandika: “Machipukizi ya spishi za Yucca huliwa na Wahindi wa Amerika wenyeji, na matunda na mizizi inaweza kutumiwa kama sabuni ya kufulia nguo.” Waamerika wa Kati wametumia ifaavyo manufaa ya kiasili ya yucca ya kuweza kupikika na kusafishia. Wao hupendezwa kwa kadiri fulani na ladha yake yenye gwadu na bado iliyo kali. Maua yake hutumiwa kutengenezea kachumbari au hupikwa pamoja na mayai na viazi, mlo upendwao sana miongoni mwa watu wa Kosta Rika na Waamerika wengine wa Kati. Yucca ina manufaa ya lishe kwa sababu ina vitamini na madini kwa wingi, kama vile kalisi, chuma, themioni, fosforasi, na riboflavini.

      Ya kufaa kuangaliwa pia ni yale manufaa ya kitiba ya yucca; umajimaji uliotayarishwa kwa kuchemsha na kulowesha maua haya ndani ya maji hutuliza tumbo. Majani yaweza kutumiwa kutibu albuminuria na uvimbe wa utumbo mpana na yaweza kutumiwa kama dawa ya kukojoza. Na mitishamba hii, inayoweza kutumiwa kutengenezea sabuni, iliyo mitamu, na yenye lishe ni moja tu ya uumbaji wa dunia ambao seli-onji zetu zaweza kuonea shangwe!

  • Yucca Usio na Miiba—Mmea Wenye Kubadilika Isivyo Kawaida
    Amkeni!—1998 | Januari 22
    • Maua ya “yucca” yakiwa yamepikwa kwa mayai na viazi ni chakula kipendwacho sana katika Amerika ya Kati

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki