Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 1/22 kur. 26-27
  • Yucca Usio na Miiba—Mmea Wenye Kubadilika Isivyo Kawaida

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yucca Usio na Miiba—Mmea Wenye Kubadilika Isivyo Kawaida
  • Amkeni!—1998
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mshiriki wa Familia Iliyo Tofauti
  • Ni Mtamu kwa Kulika
  • Kosta Rika—Nchi Ndogo, Unamna Mwingi
    Amkeni!—1995
  • Ni Maridadi na Matamu!
    Amkeni!—2004
  • Kinywaji Chenye Kuburudisha Kutokana na Mmea wa Kigeni
    Amkeni!—2002
  • Matendo ya Mashahidi wa Yehova Katika Nyakati za Kisasa
    1988 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 1/22 kur. 26-27

Yucca Usio na Miiba—Mmea Wenye Kubadilika Isivyo Kawaida

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA KOSTA RIKA

UNAFANANA na mitishamba, unafanana na sabuni, ni mtamu na wenye lishe. Mmea huu usio wa kawaida una sifa hizi zote bainifu, na nyingine nyingi! Unajulikana vizuri na Waamerika wa Kati lakini si kwa jina yucca usio na miiba. Ikiwa ungetumia neno hilo katika Amerika ya Kati, watu wengi zaidi wangeelekea kuitikia kwa upole na kukukodolea macho yenye udadisi. Hata hivyo, tabasamu pana ya utambuzi ingeonekana mara moja ikiwa ungetaja itabo, izote, au daguillo, kama mmea huo ujulikanavyo kikawaida katika Kosta Rika, Guatemala, Honduras, na Nikaragua. Watu wa Kosta Rika na Waamerika wengine wa Kati hufurahia ladha ya maua yake katika vyakula vya namna nyingi.

Mshiriki wa Familia Iliyo Tofauti

Katika ule unaoonekana kuwa mvutano, yucca usio na miiba umeorodheshwa na wanauainishaji kama mshiriki wa familia ya Lilaki na hivi karibuni kama mshiriki wa familia ya Mkongepori. Hiyo familia ya mwisho ya mimea isiyo laini hujumuisha spishi kadhaa 550 kutoka kikundi cha Yungiyungi. Wanabotania wametambulisha jina lake la kisayansi kuwa Yucca elephantipes.

Inakadiriwa kuna spishi 40 za Yucca zenye sifa zinazofanana, ambazo nyingi za hizo hupatikana katika Amerika Kaskazini, Mexico, na Amerika ya Kati na ya Kusini. Jamaa wanaojulikana vizuri wanatia ndani ule mti mkubwa Joshua (Yucca brevifolia) na ule mdogo wa Kihispania wenye umbo-singe (Yucca aloifolia). Kwa kweli ni familia kubwa!

Ni zipi baadhi ya sehemu kuu zinazotofautisha mmea huu wenye matumizi mengi? Ovyoovyo na bado si ya kawaida katika sura, majani yake magumu, na yaliyorefuka hunyooka kufikia meta moja kutoka kwenye shina. Hilo shina nene na lenye miti, pamoja na umbile lake la nyuzinyuzi na rangi ya kijivujivu-kahawia, hufanana na mguu wa mbele wa tembo—hivyo, jina la kisayansi elephantipes.

Unapoutupia jicho mara ya kwanza, yucca usio na miiba, unaofikia kimo cha meta 4 hadi 7, waweza kukosewa kwa urahisi kuwa mti. Wakati wa msimu wa kiangazi katika Kosta Rika, hasa miezi ya Februari na Machi, mamia ya maua ya rangi ya pembe ya ndovu, yenye umbo la kengele, huvika taji mmea wa itabo. Inaonekana kuwa mahali pote kwa wakati uleule kwa kuwa inauzwa mahali pa soko na wachuuzi wa barabarani! Kwa kutofautisha kabisa na majani magumu, yenye umbo la singe, maua haya mororo huchanua katika kishada yakikua barabara katikati ya mmea, na yakiwa wima.

Hii itabo ni mojawapo spishi za yucca zipendwazo zaidi na watunza-bustani pamoja na wasanifu-mandhari, kwa kuwa hubadilikana ili kufaana na namna mbalimbali za tabia ya nchi na udongo na kutokeza sura ya kitropiki, isiyo ya kawaida. Wakati mmoja ulitumiwa kama ua wa asili wa kuweka mipaka ya ardhi katika Kosta Rika, si ajabu kwamba mti huu itabo wenye kuzaa sana ni mwingi sana karibu katika kila eneo la nchi.

Bila shaka wenyeji wa hapo wamefaidika na matumizi mengi ya mti huu. Kwa mfano, nyuzi zinazotolewa kutoka kwenye majani zinatumiwa kutengenezea mikeka, mishipi, na shanta. Pia, ikiwa majani yanapatwa na joto lililo la kiwango kilekile, watunza-bustani wanaweza kuyatumia kama kamba za kufungia mazao yao. Yaonekana kana kwamba hakuna mwisho wa matumizi ya mmea huu!

Ni Mtamu kwa Kulika

Frances Perry, mtungaji wa Flowers of the World, aandika: “Machipukizi ya spishi za Yucca huliwa na Wahindi wa Amerika wenyeji, na matunda na mizizi inaweza kutumiwa kama sabuni ya kufulia nguo.” Waamerika wa Kati wametumia ifaavyo manufaa ya kiasili ya yucca ya kuweza kupikika na kusafishia. Wao hupendezwa kwa kadiri fulani na ladha yake yenye gwadu na bado iliyo kali. Maua yake hutumiwa kutengenezea kachumbari au hupikwa pamoja na mayai na viazi, mlo upendwao sana miongoni mwa watu wa Kosta Rika na Waamerika wengine wa Kati. Yucca ina manufaa ya lishe kwa sababu ina vitamini na madini kwa wingi, kama vile kalisi, chuma, themioni, fosforasi, na riboflavini.

Ya kufaa kuangaliwa pia ni yale manufaa ya kitiba ya yucca; umajimaji uliotayarishwa kwa kuchemsha na kulowesha maua haya ndani ya maji hutuliza tumbo. Majani yaweza kutumiwa kutibu albuminuria na uvimbe wa utumbo mpana na yaweza kutumiwa kama dawa ya kukojoza. Na mitishamba hii, inayoweza kutumiwa kutengenezea sabuni, iliyo mitamu, na yenye lishe ni moja tu ya uumbaji wa dunia ambao seli-onji zetu zaweza kuonea shangwe!

[Picha katika ukurasa wa 26]

Maua ya “yucca” yakiwa yamepikwa kwa mayai na viazi ni chakula kipendwacho sana katika Amerika ya Kati

[Picha katika ukurasa wa 27]

“Yucca” zinazokua mashambani hufanana na miti

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki