Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jinsi ya Kujilinda Dhidi ya Ulaghai
    Amkeni!—2004 | Julai 22
    • Mbinu moja inayotumiwa sana ni ile ya kuwahusisha watu wengi katika biashara na kuwaahidi kuwa watatajirika haraka. Ingawa mbinu hiyo hutumiwa kwa njia mbalimbali, kwa kawaida wahusika huwatafuta watu wengine wa kujiunga na biashara hiyo, na wanapofanya hivyo wanalipwa.b Mbinu nyingine inahusisha kuwatumia watu kadhaa barua yenye majina na kuwaomba wamtumie pesa mtu wa kwanza kwenye orodha hiyo ya majina. Mtu huahidiwa kwamba atapokea maelfu ya dola wakati jina lake litakapokuwa la kwanza kwenye orodha hiyo.

      Sikuzote biashara hizo huanguka kwa kuwa haiwezekani kuendelea kuwatafuta washiriki wapya. Fikiria mfano unaofuata. Ikiwa watu watano wangeanzisha mradi wa biashara kisha kila mmoja wao awatafute watu watano zaidi, biashara hiyo itakuwa na watu 25 zaidi. Kila mmoja wao akitafuta watu 5 zaidi, watu 125 wataongezwa. Wakifanya hivyo mara tisa, biashara hiyo itakuwa na watu milioni mbili hivi, nao watatafuta zaidi ya watu milioni tisa! Wasimamizi wa miradi hiyo wanajua kwamba kuna kiwango ambacho hakiwezi kupitwa. Wanapogundua kwamba wanakaribia kufikia kiwango hicho, wao hutoroka na pesa. Huenda ukapoteza pesa zako, na watu ambao umewashawishi kujiunga na biashara hiyo watakudai pesa zao. Kumbuka kwamba, katika mradi kama huo, ili upate pesa, ni lazima mtu mwingine apoteze pesa.

  • Jinsi ya Kujilinda Dhidi ya Ulaghai
    Amkeni!—2004 | Julai 22
    • b Huu ni mradi mkubwa wa biashara ambapo watu hulipa kiasi fulani cha pesa ili wajiunge na kuwatafuta watu wengine wanaotaka kujiunga na biashara hiyo. Mara nyingi biashara za aina hiyo hazitoi huduma wala bidhaa zozote.

  • Jinsi ya Kujilinda Dhidi ya Ulaghai
    Amkeni!—2004 | Julai 22
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 8, 9]

      Mbinu Sita Zinazotumiwa Kwenye Barua-pepe

      1. Biashara za kuwatafuta washiriki wapya: Biashara hizo huonwa kuwa njia ya kujitajirisha bila jitihada yoyote wala kutumia pesa nyingi. Watu wengine hupewa kompyuta au kifaa kingine cha elektroni wanapolipa pesa za kujiunga na biashara hizo na kutafuta washiriki wengine. Wakati mwingine watu hutumiwa barua zenye orodha ya majina. Mara nyingi barua hizo si halali. Watu wengi wanaojiingiza katika biashara hizo hupoteza pesa zao.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki