Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 2/22 uku. 32
  • Faraja kwa Familia na Marafiki

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Faraja kwa Familia na Marafiki
  • Amkeni!—1997
Amkeni!—1997
g97 2/22 uku. 32

Faraja kwa Familia na Marafiki

NDEGE nambari 800 ya shirika la ndege la TWA ilipoanguka katika Bahari-Kuu ya Atlantiki katika Julai 17, watu wote 230 waliokuwamo walikufa. Hao walitia ndani wanafunzi 16 wa shule ya sekondari waliokuwa wakijifunza Kifaransa na wasimamizi watano walio watu wazima ambao walitoka Montoursville, mji mdogo katika Pennsylvania wenye wakazi wapatao 5,000. Katika mkutano mmoja wa ukumbusho uliofanywa mjini mnamo Agosti 17, mmoja wa wasemaji, Rudolph Giuliani, meya wa New York City, alisema kwamba kama asilimia hiyohiyo ya wakazi wa New York City ingekufa, watu 35,000 wangekufa!

Mkuu wa shule hiyo ya sekondari, Dan Chandler, aliombwa atoe hotuba katika maziko ya wanafunzi kadhaa. Yeye alinukuu ahadi ya Biblia kwenye Ufunuo 21:4, isemayo kwamba katika mfumo mpya wa mambo wa Mungu “kifo hakitakuwapo tena, wala ombolezo wala kupaaza kilio wala umivu halitakuwapo tena kamwe.” Kuhusu ni kwa nini misiba kama hii hutukia, yeye alitaja Mhubiri 9:11 (NW), lisemalo juu ya “wakati na tukio lisilotazamiwa” likitupata sisi sote. Wengi walishangaa kumsikia mkuu wao wa shule akisema maneno yenye kufariji hivyo.

Ili kutoa msaada zaidi, Chandler aliandaa meza kwenye shule hiyo ya sekondari ambamo aliweka vichapo kama broshua yenye kurasa 32 Mtu Fulani Umpendaye Anapokufa na trakti Kuna Tumaini Gani kwa Wapendwa Waliokufa? Mamia ya fasihi ya Biblia yalichukuliwa, na wengi walishukuru kwa faraja ambayo fasihi hizo ziliandaa.

Wewe pia waweza kupata faraja kutokana na broshua na trakti hizo ambazo zimetajwa hapo juu. Kama ungependa kupokea nakala ya kila moja au kuwa na funzo la Biblia nyumbani bila malipo, tafadhali andikia I.B.S.A., P. O. Box 47788, Nairobi, Kenya, au kwa kutumia anwani ihusuyo kwenye ukurasa 5.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]

Kwa hisani ya Williamsport Sun-Gazette

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]

Corey Sipkin/Sipa Press

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki