-
Yehova Amekuwa Kimbilio LanguMnara wa Mlinzi—1996 | Desemba 1
-
-
Tulikuwa na tamaa yenye nguvu ya kusema na wengine kuhusu mambo tuliyokuwa tukijifunza, kwa hiyo tukaanza katika huduma ya mlango hadi mlango kwa kutumia ile trakti Message of Hope.
-
-
Yehova Amekuwa Kimbilio LanguMnara wa Mlinzi—1996 | Desemba 1
-
-
Tulipogawanya ile trakti Message of Hope, watoto walikusanyika kutuzunguka wakipaaza sauti “Wamileani” na maneno mengine ya kuvunja heshima. Wafanyakazi wenzi wa mume wangu wakaanza pia kumletea matata. Mwisho-mwisho wa mwaka 1926 alifikishwa mahakamani, akashtakiwa kuwa hafai kuwa mwalimu wa shule ya umma, na kuhukumiwa kifungo cha siku 15 gerezani.
Mama alipopata kujua hilo, alinisihi nimwache mume wangu. “Sikiliza, mamangu mpendwa,” nikajibu, “wajua kadiri nijuavyo jinsi ninavyokupenda na kukustahi. Lakini siwezi kwa vyovyote kukuruhusu utuzuie tusimwabudu Mungu wa kweli, Yehova.” Alirudi kijijini kwake akiwa ametamauka sana.
-