Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Guyana
    2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Katika muda wa majuma mawili tu, mwangalizi mmoja wa mzunguko alionyesha sinema hiyo mara 17. Mara nyingi aliionyesha nje, na watu 5,000 waliitazama.

      “Pindi nyingine, mwangalizi mmoja wa mzunguko alisafiri kwa muda wa siku mbili kwenye mto wenye maporomoko, kisha akatembea kwa miguu kwenye kijia cha msitu kwenda kuonyesha sinema hiyo. Jitihada zake hazikuwa za bure kwa kuwa Wahindi wenyeji wengi, ambao hawakuwa wamewahi kuona sinema, waliifurahia. Siku iliyofuata, wanakijiji wengi ambao walikuwa wafuasi wa kanisa la Presbiteri, walichukua magazeti. Baada ya ziara hiyo, watu wote wa kijiji hicho walikuwa na maoni mazuri kuwahusu watu wa Yehova.”

  • Guyana
    2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Alan Johnstone, mhitimu wa Shule ya Gileadi aliyekuja Guyana mwaka wa 1957 na kutumikia akiwa mwangalizi wa mzunguko, alionyesha sinema hiyo pindi kadhaa. Anaandika: “Mahali ambapo hapakuwa na umeme, kwa fadhili wenyeji walituazima jenereta zao ambazo walitumia kuangazia maduka yao usiku. Ili kuonyesha sinema hiyo tulitandaza shuka kubwa kati ya miti miwili.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki