-
Guyana2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Mapainia Wenyeji Wahudhuria Shule ya Gileadi
Mapainia kadhaa wenyeji walipata pia pendeleo la kuhudhuria Shule ya Gileadi, na baadhi yao wakarudi Guyana. Baadhi ya mapainia hao ni Florence Thom (sasa anaitwa Brissett), darasa la 21, 1953;
-
-
Guyana2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Florence Brissett anasema: “Nilitarajia kutumwa katika nchi za kigeni, lakini niliiona kuwa baraka kutoka kwa Yehova nilipotumwa katika kijiji cha Skeldon, nchini Guyana. Wengi kati ya wanashule wenzangu wa zamani, walimu, marafiki, na watu niliofahamiana nao walikubali kujifunza Biblia pamoja nami kwa sababu walinijua. Hata wengine, kama vile Edward King ambaye mke wake alikuwa akijifunza pamoja nami, waliniomba nijifunze Biblia pamoja nao! Kasisi wa Kanisa la Anglikana aliposikia kwamba mke wa Edward alikuwa akijifunza, alimwita Edward na kumwamuru asimamishe funzo hilo mara moja. Lakini badala ya kufanya hivyo, Edward mwenyewe alianza kujifunza.”
-