-
Guyana2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Waangalizi wa mzunguko pia walipatwa na mikasa. Jerry na Delma Murray, waliokuwa wakisafiri kwa pikipiki, walifika kwenye mtaro fulani ambao daraja lake lilikuwa limetengenezwa kwa mbao chache zilizounganishwa pamoja. Delma alingoja huku Jerry akivuka daraja hilo kwa pikipiki. Lakini wakati wa kuvuka mambo yalienda mrama, na Jerry akatumbukia kwenye maji yenye matope pamoja na pikipiki na sanduku. Delma alipiga mayowe na wanakijiji wakaja mbio kusaidia. Muda mfupi baadaye, wasiwasi uligeuka kuwa kicheko kwa kuwa, kama vile ndugu mmoja alivyoandika, “mzungu huyo alipanda ufuoni akiwa amefunikwa na magugu, na viatu vikiwa vimejaa matope.”
-
-
Guyana2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Picha katika ukurasa wa 175]
Jerry na Delma Murray
-