Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Guyana
    2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Katika Aprili mwaka wa 1946, Nathan Knorr kutoka makao makuu alitembelea Guyana. Aliandamana na William Tracy, aliyekuwa amehitimu Shule ya Gileadi muda mfupi kabla ya hapo. Walikuja ili kuwatia ndugu moyo na kuiomba serikali iondoe marufuku. Katika mkutano uliofanywa huko Georgetown, Ndugu Knorr aliwaeleza ndugu na watu wenye kupendezwa 180 waliokuwa wamekusanyika kwamba, wanafunzi wa zamani wa Yesu hawakuwa na Biblia wala vitabu vya kuwasaidia katika huduma. Hata hivyo, Yehova aliwabariki kwa ongezeko kubwa. Kwa nini? Kwa sababu waliendelea kuhubiri. Kwa hiyo, hapana shaka kwamba Mungu angewabariki watumishi wake wa siku hizi kama wangeendelea kuhubiri bila kuacha.

  • Guyana
    2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Ndugu Knorr pia alimtembelea W. L. Heape, aliyekuwa waziri wa koloni hiyo na kuomba marufuku iondolewe. Baada ya mazungumzo yao ya dakika 30, Ndugu Knorr alimpa Bw. Heape nakala ya kitabu kimoja cha funzo (“The Truth Shall Make You Free”), naye akamwomba akisome kwa makini. Bw. Heape alisema kwamba atakisoma. Isitoshe, alimwambia Ndugu Knorr kwamba marufuku juu ya vichapo vyetu ilikuwa ikizungumziwa na wanachama tisa wa kamati ya usimamizi wakati huohuo! Bw. Heape alisema kweli, kwa kuwa mnamo Juni 1946, gavana alitangaza kuondolewa kwa marufuku hiyo.

  • Guyana
    2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 146]

      Frederick Phillips, Nathan Knorr, na William Tracy, mwaka wa 1946

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki