Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 1/8 uku. 32
  • “Amkeni! Liliokoa Maisha Yangu”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Amkeni! Liliokoa Maisha Yangu”
  • Amkeni!—1998
Amkeni!—1998
g98 1/8 uku. 32

“Amkeni! Liliokoa Maisha Yangu”

“Karibu saa nne za usiku katika Novemba 11,” akaripoti Arthur, katika Suva, Fiji, “nilianza kuhisi maumivu ya kifua, ambayo nilidhani kuwa ni uchungu wa kiungulia. Mke wangu, Esther, alisadiki kwamba nilikuwa napatwa na mshiko wa moyo, kwa kuwa alisema dalili zangu zilifanana na zile zilizofafanuliwa katika Amkeni! la Desemba 8, 1996, “Maradhi ya Moyo—Ni Nini Kinachoweza Kufanywa?,” ambalo alitoka tu kusoma.

“Niliongea na daktari wangu kwenye simu, akanishauri nitumie dawa fulani za kiungulia, nilale usingizi, na kumwona asubuhi. Na bado, maumivu yaliendelea. Kisha nilimwomba Esther alete lile Amkeni! na kusoma ile sehemu “Dalili za Mshiko wa Moyo.” Baada ya kunisomea sehemu hiyo, nilikubali kupelekwa hospitalini.

“Upimaji ulionyesha kwamba nilikuwa napatwa na mshiko wa moyo, nikalazwa hospitalini. Kwa siku tano zilizofuata, nilipewa dawa nyingi za kunituliza na kuagizwa nipumzike kikamili. Mtaalamu wa moyo aliniambia ilikuwa vizuri kwamba niligundua mshiko wa moyo wangu.

“Katika Januari 9, 1997, nilifanyiwa upasuaji wa moyo uliochukua muda wa saa nne katika Sydney, Australia. ‘Maradhi hayo ya ateri ya moyo yalikuwa mabaya sana,’ ikataarifu ripoti ya daktari-mpasuaji. Hali ya ateri za moyo wangu ilionyesha kwamba ningalikuwa na mshiko mkubwa wa moyo ambao ungalikuja kwa miezi michache iwapo ule mshiko wa Novemba 11 haungaligunduliwa.

“Naweza kusema bila shaka kwamba lile Amkeni! liliokoa maisha yangu, kwa kuwa kwa wazi ningalichukulia mshiko wangu kuwa maumivu makali ya kiungulia.”

Amkeni! hujitahidi sana kutoa habari kwa wakati unaofaa na ya karibuni juu ya mambo mbalimbali. Ikiwa ungependa kupokea jarida hili kwa ukawaida, uwajulishe Mashahidi wa Yehova wakati ufuatao watakapokutembelea, au andika kwa kutumia anwani ihusuyo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki