Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maradhi ya Moyo—Tisho kwa Uhai
    Amkeni!—1996 | Desemba 8
    • Maradhi yaweza kuathiri sehemu yoyote ya moyo. Hata hivyo, maradhi ya kawaida zaidi ni yale ya kudhuru kichini-chini yapatayo mishipa ya moyo ambayo huitwa atherosclerosis. Maradhi hayo yatokeapo, mkusanyo wa mafuta, hukua katika kuta za ateri. Baada ya kipindi fulani, mkusanyo huo waweza kuongezeka na kuwa mgumu, kujaa ndani ya ateri, na kuziba mtiririko wa damu inayoenda moyoni. Ni maradhi haya ya ateri ya moyo (CAD) ambayo husababisha mishiko mingi sana ya moyo.

      Kuziba kwa ateri moja au zaidi huharakisha shambulio moyo unapopungukiwa oksijeni. Hata katika ateri ambazo hazijazibwa sana, mkusanyo wa mafuta waweza kuvunjika vipande-vipande na kufanyiza mgando wa damu (thrombus). Ateri zenye maradhi pia huathiriwa kwa urahisi na mpindano. Mgando wa damu waweza kujifanyiza mahali pa mpindano, ukitokeza kemikali ambayo huzidi kubana ukuta wa ateri, jambo ambalo hutokeza mshiko wa moyo.

  • Kutambua Dalili na Kuchukua Hatua
    Amkeni!—1996 | Desemba 8
    • Kati ya wengi ambao wana dalili za CAD, Harvard Health Letter yaripoti, karibu nusu wataahirisha kutafuta msaada wa kitiba. Kwa nini? “Mara nyingi kwa sababu hawatambui dalili hizo ni za nini au hawazichukui kwa uzito.”

      John,a ambaye ni mhasiriwa wa mshiko wa moyo na ambaye pia ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova, asihi hivi: “Unapohisi kwamba kuna kasoro, usikawie kupata tiba kwa hofu ya kwamba utaonekana unatilia chumvi ugonjwa wako. Karibu nife kwa sababu sikuchukua hatua haraka iwezekanavyo.”

      Kile Kilichotendeka

      John aeleza: “Mwaka mmoja na nusu kabla ya kupatwa na mshiko wa moyo, nilionywa na daktari kuhusu kolesteroli nyingi niliyokuwa nayo, ambayo ni kisababishi kikuu cha CAD. Lakini niliepuka suala hilo, kwa kuwa nilihisi kwamba nilikuwa mchanga—chini ya umri wa miaka 40—na mwenye afya nzuri. Nasikitika sana kwamba sikuchukua hatua wakati huo. Nikapata ishara nyinginezo za kuonya—kukosa pumzi nikijikakamua kidogo tu, maumivu ambayo niliyafikiria kuwa tatizo la umeng’enyaji wa chakula na, kwa miezi kadhaa kabla ya kupatwa na mshiko wa moyo nilikuwa mchovu mno. Nilifikiri kwamba nyingi za dalili hizo zilitokezwa na ukosefu wa usingizi na mkazo mwingi sana wa kazi. Siku tatu kabla ya kupatwa na mshiko wa moyo, nilihisi kile nilichokifikiria kuwa mpindano wa misuli katika kifua changu. Huo ulikuwa mshiko mdogo wa moyo ambao ulitangulia mshiko mkubwa ulionipata siku tatu baadaye.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki