Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Tumaini Zuri Zaidi kwa Ajili ya Nafsi
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Agosti 1
    • b Bila shaka, sawa na maneno mengi yawezayo kutumiwa kwa njia nyingi sana, neno neʹphesh pia lina maana mbalimbali. Kwa mfano, yaweza kurejezea mtu wa ndani, hasa katika kurejezea hisia zenye kina. (1 Samweli 18:1) Yaweza kurejezea pia maisha ambayo mtu hufurahia akiwa nafsi.—1 Wafalme 17:21-23.

  • Tumaini Zuri Zaidi kwa Ajili ya Nafsi
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Agosti 1
    • Kwa neno moja, la. Mlemle katika kitabu cha kwanza chenyewe cha Biblia, Mwanzo, tunaambiwa kwamba nafsi si kitu fulani ulicho nacho, hiyo ni wewe mwenyewe. Twasoma hivi juu ya uumbaji wa Adamu, yule binadamu wa kwanza: “Mtu akawa nafsi hai.” (Mwanzo 2:7, italiki ni zetu.) Neno la Kiebrania linalotumiwa hapa kwa nafsi, neʹphesh, huonekana zaidi ya mara 700 katika Maandiko ya Kiebrania, bila kuonyesha kamwe hata mara moja wazo la kwamba kuna sehemu ya kiroho ya mwanadamu, iliyotengwa, iliyo ya kimbingu. Kinyume cha hilo, nafsi ni ya kugusika, ya kushikika, halisi.

      Fungua katika nakala yako mwenyewe ya Biblia, maandiko yafuatayo yaliyotajwa, kwani neno la Kiebrania neʹphesh linapatikana katika kila moja yayo. Yanaonyesha kwa wazi kwamba nafsi yaweza kukabili tisho, hatari, na hata kutekwa nyara (Kumbukumbu la Torati 24:7; Waamuzi 9:17; 1 Samweli 19:11); kugusa vitu (Ayubu 6:7); kutiwa katika minyororo ya chuma (Zaburi 105:18); kutamani kula, kuteswa kwa kufunga, na kuzimia kwa sababu ya njaa na kiu; na kupatwa na ugonjwa wenye kudhoofisha au hata hali ya kukosa usingizi kwa sababu ya huzuni. (Kumbukumbu la Torati 12:20; Zaburi 35:13; 69:10; 106:15; 107:9; 119:28) Yaani, kwa sababu nafsi yako ni wewe, wewe binafsi, nafsi yako yaweza kupatwa na jambo lolote uwezalo kupatwa nalo.b

  • Tumaini Zuri Zaidi kwa Ajili ya Nafsi
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Agosti 1
    • Si ajabu sana kwamba The Encyclopedia Americana husema hivi juu ya nafsi katika Maandiko ya Kiebrania: “Dhana juu ya binadamu iliyo katika Agano la Kale ni ile ya muungano, si kufungamana kwa nafsi na mwili.” Yaongeza hivi: “Nefesh . . . haionwi kamwe kuwa yenye kutenda kazi kando ya mwili.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki