Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Unapokumbwa na Ugonjwa
    Amkeni!—2001 | Januari 22
    • Unapokumbwa na Ugonjwa

      John, baada ya kugundua kwamba alikuwa na ugonjwa wenye kudhoofisha—“Nilishtuka sana.”

      Beth, baada ya kufahamu hatari ya ugonjwa wake.—“Nilihofu sana.”

      KUFAHAMU kwamba una ugonjwa wa kudumu au wa kulemaza au kufahamu kwamba utalemaa kabisa kwa sababu ya majeraha uliyoyapata katika aksidenti ni mojawapo ya mambo yenye kuhuzunisha zaidi maishani. Iwe utapokea habari za ugonjwa wako katika ofisi tulivu ya daktari au utagundua ulemavu wako katika chumba cha tiba ya dharura chenye hekaheka, yamkini utapigwa na bumbuazi. Maisha hayakutayarishi kukabiliana na hisia-moyo kali zinazokukumba wakati unaposhikwa na tatizo baya sana la kiafya.

      Ili kukusanya habari ambazo zaweza kuwasaidia wale ambao afya yao imezorota vibaya hivi karibuni, Amkeni! liliwahoji watu kadhaa kutoka nchi mbalimbali ambao wamekabiliana kwa mafanikio na ugonjwa wa kudumu wenye kulemaza kwa miaka mingi. Waliombwa watoe maoni yao kwa maswali kama vile: Ulihisije? Ni nini kilichokusaidia ustahimili tatizo hilo na kupata usawaziko tena? Ulichukua hatua gani ili kudhibiti tena maisha yako kwa njia fulani? Habari yenye kuarifu kutoka kwa mahoji hayo ya moja kwa moja na vilevile matokeo ya watafiti ambao wanachunguza athari za magonjwa ya kudumu yameandikwa ili kuwanufaisha wale wanaokabili ugonjwa hivi sasa.a

  • Kufadhaishwa na Hisia-Moyo
    Amkeni!—2001 | Januari 22
    • Kufadhaishwa na Hisia-Moyo

      “BAADA ya kuambiwa kwamba nilikuwa na ugonjwa wenye kufisha,” akumbuka mwanamume mmoja mzeemzee, “nilijaribu kushinda hofu yangu, lakini hisia za shaka zilinilemea.” Maneno yake yakazia uhakika wa kwamba ugonjwa mbaya haumlemazi mtu kimwili tu bali pia humwumiza kihisia. Hata hivyo, kuna watu ambao wanakabiliana kwa mafanikio na hali hizo. Wengi wao wangependa kukuhakikishia kwamba kuna njia za kukabiliana kwa mafanikio na ugonjwa wenye kudumu.

  • Kufadhaishwa na Hisia-Moyo
    Amkeni!—2001 | Januari 22
    • “Nyakati nyingine, hali yangu isiyojulikana hufanya maisha yawe yenye kutamausha sana,” asema mwanamume mwenye ugonjwa wa kutetemeka. “Kila siku, nina wasiwasi kuhusu hali yangu.”

  • Kufadhaishwa na Hisia-Moyo
    Amkeni!—2001 | Januari 22
    • Mtu mmoja aliyepooza akumbuka hivi: “Niliaibika sana kwamba nilipatwa na hali hiyo kwa sababu ya aksidenti moja ya kipumbavu!”

  • Kufadhaishwa na Hisia-Moyo
    Amkeni!—2001 | Januari 22
    • Mwanamke mmoja mwenye kansa alisema hivi kwa ufupi kuhusu mawazo na hisia zake: “Baada ya kutokubali hali yangu nilishikwa na hasira kali kisha nikaanza kutafuta msaada.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki