-
Matukio Muhimu ya mwaka uliopita2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Italia
Wahubiri 7,200 wamejifunza lugha 18 tofauti-tofauti. Mmoja wa wanafunzi hao alikutana na Samson anayetoka nchi ambako kazi ya kuhubiri ujumbe wa Ufalme imepigwa marufuku. Alipokuwa na miaka 24, Samson alifunga safari ambayo aliiita safari ya tumaini. Kwanza alivuka jangwa, kisha akasafiri kwa meli hadi Italia. Samson alipofika Italia alikutana na yule mwanafunzi ambaye alikuwa amejifunza lugha yake. Samson alisikiliza kwa makini na hata akahudhuria mkutano wa Kikristo. Baada ya kupoteana kwa miezi kumi walikutana tena, na yule ndugu akaanza kujifunza Biblia pamoja na Samson. Walijifunza katika mikahawa, vituo vya gari-moshi vya chini ya ardhi, na maegesho ya magari. Baada ya kuhudhuria Ukumbusho, Samson alianza kufanya mabadiliko maishani, hata alivunja uhusiano na mwanamke aliyekuwa ameishi naye kwa mwaka mmoja. Sasa yeye ni ndugu yetu.
-
-
Matukio Muhimu ya mwaka uliopita2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Picha katika ukurasa wa 20]
Darasa la Kihispania, Rome, Italia
[Picha katika ukurasa wa 20]
Samson akihubiriwa
-