-
Kuhubiri Hadharani na Kutoka Nyumba Hadi NyumbaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Katika kipindi hicho pia kulikuwa na utangazaji mwingi kwa kutumia matangazo yaliyovaliwa na Mashahidi katika maeneo ya biashara huku wakigawanya mialiko kwa mihadhara ya pekee. Utangazaji huo ulianza katika 1936, katika Glasgow, Scotland. Mwaka huo njia ileile ya utangazaji ilitumiwa katika London, Uingereza, na kisha katika Marekani. Miaka miwili baadaye utangazaji huo uliongezwa kwa kubeba mabango yaliyoinuliwa juu kwa vijiti. Mabango hayo yalipiga mbiu, “Dini Ni Mtego na Hila”b na, “Mtumikie Mungu na Kristo Mfalme.” Wakati wa mkusanyiko, msururu wa wapiga-miguu wanaobeba mabango hayo ungeweza kuwa na urefu wa kilometa nyingi. Walipopiga miguu bila kelele, mmoja akimfuata mwingine, huku wakipitia barabara zenye wasafiri wengi, tokeo lilikuwa kama lile la jeshi la Israeli la kale likizunguka Yeriko kabla kuta zalo kuanguka. (Yos. 6:10, 15-21)
-
-
Kuhubiri Hadharani na Kutoka Nyumba Hadi NyumbaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
[Picha katika ukurasa wa 568]
Matangazo kwa mabango na ishara zilichangia kutoa ushahidi hadharani kwa ujasiri (kama hapa katika Scotland)
-