-
Latvia2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Wakati huo, kulikuwa na wahubiri wa Ufalme chini ya 50 nchini. Hata hivyo, ili waendeshe mambo kisheria, akina ndugu walituma maombi ya kusajiliwa. Wazia jinsi walivyoshangilia wakati shirika la International Bible Students Association liliposajiliwa rasmi Machi 14, 1933! Ingawa hawakuruhusiwa kuingiza vichapo vya Biblia nchini, akina ndugu walitumia haki yao ya kisheria kuchapisha vijitabu fulani nchini. Aleksandrs Grīns, mwandishi maarufu na mhariri mkuu wa gazeti la Rīts, alitafsiri vichapo katika Kilatvia.
-
-
Latvia2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
USAJILI HAUKUDUMU
Mapinduzi yaliyotukia Mei 1934, yalifanya sheria za kijeshi zianze kutumiwa. Maadui wa ile kweli walitumia msukosuko huo wa kisiasa kuwashtaki watu wa Mungu kuwa Wakomunisti. Mnamo Juni 30, waziri wa mambo ya ndani alifunga ofisi ya shirika la International Bible Students Association na kuchukua vitabu na vijitabu zaidi ya 40,000 na kiasi kidogo cha pesa. Makasisi walipewa kazi ya kufunga hesabu za ofisi hiyo! Maombi ya kusajiliwa upya yalikataliwa.
-