-
Yerusalemu Na Hekalu La Sulemani‘Ona Nchi Nzuri’
-
-
Yerusalemu Na Hekalu La Sulemani
LILIITWA “ukamilifu wa uzuri” na “mji wa Mfalme Mkuu.” (Zb 48:2; 50:2; Omb 2:15) Yerusalemu lilikuwa jiji kuu la taifa la Mungu. (Zb 76:2) Baada ya Daudi kuteka jiji hilo kutoka kwa Wayebusi na kulifanya kuwa jiji lake kuu, liliitwa “Jiji la Daudi,” au “Sayuni.”—2Sa 5:7.
Ingawa Yerusalemu halikuwa mahali muhimu kivita, lilikuwa mashuhuri kwa sababu Mungu aliweka jina lake hapo. (Kum 26:2) Lilikuwa kituo cha kidini na cha kuendesha shughuli za serikali.
Yerusalemu liko katika mwinuko wa meta 750 juu ya usawa wa bahari katika safu ya milima iliyo katikati mwa Yudea. Biblia inataja kwamba jiji hilo lilikuwa ‘limeinuka’ na waabudu ‘walipanda’ kuelekea huko. (Zb 48:2, Union Version; 122:3, 4) Jiji hilo la kale lilizungukwa na mabonde: Bonde la Hinomu upande wa magharibi na kusini, na bonde la mto la Kidroni upande wa mashariki. (2Fa 23:10; Yer 31:40) Bubujiko la maji la Gihonia katika Bonde la Kidroni na En-rogeli lililokuwa upande wa kusini, lilikuwa chemchemi muhimu ya maji safi kwa jiji hilo hasa wakati maadui waliposhambulia.—2Sa 17:17.
Kwenye mchoro ulio katika ukurasa wa 21, Jiji la Daudi limeonyeshwa kwa rangi nyekundu. Wakati wa utawala wa Daudi na Sulemani, upande wa kaskazini wa jiji hilo ulifikia Ofeli (rangi ya kijani-kibichi) na Mlima Moria (rangi ya buluu). (2Sa 5:7-9; 24:16-25) Sulemani alimjengea Yehova hekalu lenye fahari kwenye mlima huo. Hebu wazia umati wa waabudu wakielekea “mlima wa Yehova” kwa ajili ya sherehe za kila mwaka! (Zek 8:3) Barabara zinazoonyeshwa kwenye ukurasa wa 17 zilifanya iwe rahisi kwa watu kusafiri.
-
-
Yerusalemu Na Hekalu La Sulemani‘Ona Nchi Nzuri’
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 21]
Baada ya muda, mipaka ya Yerusalemu ilipanuka upande wa magharibi na kaskazini. Wafalme wa Yuda waliotawala baada ya Sulemani walijenga kuta na malango zaidi. Utafiti wa kiakiolojia unaoendelea huenda ukaonyesha waziwazi ukubwa wa baadhi ya kuta hizo na mahali hususa zilipokuwa. Jiji hilo liliharibiwa mwaka wa 607 K.W.K. na likabaki ukiwa kwa miaka 70. Miaka 80 hivi baada ya Wayahudi kurudi, Nehemia alianza kazi kubwa sana ya kujenga upya kuta za Yerusalemu.
-