Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Huwabariki na Kuwalinda Wale Wanaomtii
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Oktoba 1
    • Waliotii Waliokoka Wakati wa Mazingiwa

      16. Yehova aliwaonyeshaje huruma Wayahudi waliokuwa Yerusalemu wakati wa mazingiwa yaliyofanywa na Wababiloni mwaka wa 607 K.W.K.?

      16 Yerusalemu lilipoharibiwa mwaka wa 607 K.W.K., Mungu alionyesha huruma yake tena kwa waliotii. Mazingiwa yalipopamba moto, Yehova aliwaambia hivi Wayahudi: “Tazama naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti. Yeye atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; bali yeye atakayetoka, na kujitia pamoja na Wakaldayo wanaowahusuru, yeye ataishi, na maisha yake yatakuwa nyara kwake.” (Yeremia 21:8, 9) Ingawa wakazi wa Yerusalemu walistahili kuangamizwa, Yehova aliwaonyesha huruma wale waliomtii, hata wakati huo wa dharura.b

      17. (a) Utii wa Yeremia ulijaribiwa katika njia gani mbili Yehova alipomwagiza awaambie Wayahudi waliozingirwa ‘wawakimbilie Wakaldayo’? (b) Tunaweza kunufaikaje na mfano wa Yeremia wa kutii kwa ujasiri?

      17 Bila shaka, kuwaambia Wayahudi wasalimu amri kulijaribu utii wa Yeremia pia. Sababu moja ni kwamba alikuwa na bidii kwa ajili ya jina la Mungu. Hakutaka jina hilo lishutumiwe na maadui ambao wangedai wamepata ushindi kutoka kwa sanamu zisizo na uhai. (Yeremia 50:2, 11; Maombolezo 2:16) Isitoshe, Yeremia alijua kwamba, kwa kuwaambia watu wasalimu amri, angehatarisha sana maisha yake, kwa kuwa wengi wangeelewa maneno yake kimakosa kuwa uhaini. Hata hivyo, hakujikunyata kwa woga, bali alitii na kutangaza ujumbe wa Yehova. (Yeremia 38:4, 17, 18) Kama vile Yeremia, sisi pia tunatangaza ujumbe usiopendwa na wengi. Yesu alidharauliwa kwa kutangaza ujumbe huohuo. (Isaya 53:3; Mathayo 24:9) Kwa hiyo ‘tusiwaogope wanadamu,’ bali kama Yeremia tumtii Yehova kwa ujasiri, na kumtumaini kabisa.—Mithali 29:25.

  • Yehova Huwabariki na Kuwalinda Wale Wanaomtii
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Oktoba 1
    • b Andiko la Yeremia 38:19 linaonyesha kwamba Wayahudi kadhaa ‘waliwakimbilia’ Wakaldayo kwa hiyo hawakuuawa bali walipelekwa uhamishoni. Hatujui iwapo walisalimu amri kwa kutii maneno ya Yeremia. Hata hivyo, kuokoka kwao kulithibitisha maneno ya nabii huyo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki