-
“Mambo Haya Lazima Yatukie”Mnara wa Mlinzi—1999 | Mei 1
-
-
Jeshi la Waroma lilirudi mwaka wa 70 W.K. likiongozwa na Tito, mwana wa maliki Vespasian. Ni vigumu sana kuamini yale mateso yaliyowapata Wayahudi ambao walizuiliwa katika jiji hilo.c Flavio Yosefo, ambaye alijionea mambo hayo, anaripoti kwamba kufikia wakati ambapo Waroma walilibomoa jiji, karibu Wayahudi 1,100,000 walikuwa wamekufa na 100,000 hivi wakachukuliwa mateka, na upesi wengi wa mateka hao wakaangamia kwa njia yenye kutisha kutokana na njaa au katika mahali pa michezo pa Waroma. Kwa kweli, dhiki ya kipindi cha mwaka wa 66-70 W.K. ilikuwa ndiyo kubwa kupita zote ambayo Yerusalemu na mfumo wa mambo wa Kiyahudi ulikuwa umewahi kuona au ungewahi kuona.
-
-
“Mambo Haya Lazima Yatukie”Mnara wa Mlinzi—1999 | Mei 1
-
-
c Katika kitabu History of the Jews, Profesa Graetz asema kwamba nyakati fulani Waroma waliwatundika mtini wafungwa 500 kwa siku. Baadhi ya Wayahudi waliotekwa walikatwa mikono na kurudishwa jijini. Ni hali zipi zilizokuwa humo? “Pesa zilikuwa zimepoteza thamani yake, kwa kuwa hazingeweza kununua mkate. Wanaume walipigana vibaya sana barabarani waking’ang’ania chakula chenye kuchukiza sana, vifurushi vya nyasi, kipande cha ngozi, au takataka iliyotupiwa mbwa. . . . Idadi iliyokuwa ikiongezeka haraka ya maiti zisizozikwa ilifanya hewa ya kiangazi isababishe magonjwa ya kuambukiza, na ugonjwa, njaa kuu, na upanga vikawaangamiza watu.”
-