-
Yehova—Chanzo cha Haki na Uadilifu wa KweliMnara wa Mlinzi—1998 | Agosti 1
-
-
3. Ni nini tuwezalo kujifunza kwa kuchunguza maneno ya lugha ya awali yaliyotumiwa katika Biblia kuhusu haki na uadilifu?
3 Upana wa haki ya Mungu waweza kueleweka vema kwa kufikiria jinsi maneno ya lugha ya awali yanavyotumiwa katika Biblia.a Kwa kupendeza, katika Maandiko hakuna tofauti kubwa kati ya haki na uadilifu. Kwa hakika, maneno ya Kiebrania nyakati nyingine yanatumiwa kwa ulinganifu, kama tuonavyo katika Amosi 5:24 (BHN), ambapo Yehova husihi watu wake hivi: “Acheni haki itiririke kama maji, uadilifu uwe kama mto usiokauka.” Isitoshe, mara kadhaa misemo “haki na uadilifu” huonekana pamoja kwa ajili ya mkazo.—Zaburi 33:5; Isaya 33:5; Yeremia 33:15; Ezekieli 18:21; 45:9.
4. Inamaanisha nini kudhihirisha haki, na kiwango cha mwisho cha haki ni kipi?
4 Ni maana gani inayowasilishwa kwa maneno haya ya Kiebrania na Kigiriki? Kudhihirisha haki katika maana ya Kimaandiko humaanisha kufanya yaliyo sawa, bila upendeleo. Kwa kuwa Yehova ndiye huanzisha sheria na kanuni za adili, au yaliyo sawa na yasiyo na upendeleo, jinsi Yehova afanyavyo mambo ndicho kiwango cha mwisho cha haki. Kichapo Theological Wordbook of the Old Testament hueleza kwamba neno la Kiebrania linalotafsiriwa uadilifu (tseʹdheq) “hurejezea elimu ya maadili, kiwango cha adili na bila shaka katika A[gano] la K[ale] kiwango hicho ni hali na mapenzi ya Mungu.” Hivyo, jinsi ambavyo Mungu hutumia kanuni zake, na hasa jinsi ambavyo hushughulika na wanadamu wasio wakamilifu, huonyesha umaana hasa wa haki na uadilifu wa kweli.
-
-
Yehova—Chanzo cha Haki na Uadilifu wa KweliMnara wa Mlinzi—1998 | Agosti 1
-
-
a Katika Maandiko ya Kiebrania, maneno makuu matatu yanahusika. Moja ya hayo (mish·patʹ) mara nyingi hutafsiriwa kuwa “haki.” Yale mengine mawili (tseʹdheq na neno linalohusiana nalo, tsedha·qahʹ) katika visa vingi hufasiriwa kuwa “uadilifu.” Neno la Kigiriki linalotafsiriwa “uadilifu” (di·kai·o·syʹne) lafafanuliwa kuwa “sifa ya kuwa sawa au haki.”
-