Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Ni Mafundisho ya Uwongo Au ya Kweli?—Ukweli Kumhusu Yesu
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Aprili 1
    • FUNDISHO: Mamajusi watatu (au wafalme watatu kulingana na mafundisho fulani) walimtembelea Yesu baada tu ya kuzaliwa kwake.

      NI UWONGO.

      Labda umeona michoro au mandhari inayoonyesha kitoto Yesu kikiwa kimelazwa kwenye hori huku kimezungukwa na mamajusi watatu walioleta zawadi. Hata hivyo, hiyo ni mandhari ya kubuniwa tu, si ya kweli.

      Ni kweli kwamba watu fulani kutoka Mashariki walimtembelea mtoto Yesu. Hata hivyo, watu hao waliomtembelea walikuwa wanajimu, au wataalamu wa nyota. (Mathayo 2:1, Biblia Habari Njema) Je, walimpata Yesu akiwa amelazwa horini? Hapana; walimtembelea ndani ya nyumba. Yaelekea walifika miezi kadhaa baada ya Yesu kuzaliwa.—Mathayo 2:9-11.

      Yesu alitembelewa na watu wangapi? Je, walikuwa 2, 3, au 30? Biblia haisemi. Huenda wengi wanaamini kwamba ni watatu kwa sababu Biblia inataja aina tatu za zawadi.b (Mathayo 2:11) Hata watu fulani wamedokeza kwamba kila moja ya zawadi hizo inawakilisha jamii tofauti ya wanadamu. Lakini wazo hilo halipatikani katika Biblia. Badala yake, kitabu kimoja kinachofafanua vitabu vya Injili kinasema kwamba wazo hilo lilibuniwa na “mwanahistoria mbunifu sana wa karne ya nane.”

  • Je, Ni Mafundisho ya Uwongo Au ya Kweli?—Ukweli Kumhusu Yesu
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Aprili 1
    • b Mathayo anasema kwamba wageni hao “wakafungua hazina zao” na kumtolea dhahabu, ubani, na manemane. Hata hivyo, huenda familia ya Yesu—ambayo haikuwa tajiri—ilipata zawadi hizo zenye thamani kubwa wakati unaofaa kwa sababu ililazimika kukimbia nchi yao muda mfupi baadaye.—Mathayo 2:11-15.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki