Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Desturi za Krismasi-Je, Ni za Kikristo?
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Desemba 15
    • Jioni ya Januari 5, Tres Reyes Magos (“wanaume watatu wenye hekima”) wanatazamiwa kuletea watoto vichezeo.

  • Desturi za Krismasi-Je, Ni za Kikristo?
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Desemba 15
    • Katika pindi hii, nacimiento (Mandhari ya kuzaliwa kwa Kristo) huwa yenye kutokeza sana. Ni nini kinachohusika katika pindi hii? Katika sehemu za umma na vilevile makanisani na nyumbani, mandhari hujengwa yakiwa na sanamu (kubwa au ndogo) zilizotengenezwa kwa kauri, mbao, au udongo. Sanamu hizo hufananisha Yosefu na Maria wakipiga magoti mbele za hori yenye kitoto kilichotoka tu kuzaliwa. Mara nyingi kunakuwa na wachungaji na Los Reyes Magos (“wanaume wenye hekima”).

  • Desturi za Krismasi-Je, Ni za Kikristo?
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Desemba 15
    • Wakati wanaoitwa wanaume watatu wenye hekima—ambao kwa kweli walikuwa wanajimu—walipozuru Yesu na familia yao hawakuwa wakiishi tena katika hori. Muda ulikuwa umepita, na familia hiyo ilikuwa inaishi katika nyumba. Utafurahia kusoma habari kamili ya simulizi hili lililopuliziwa linalopatikana katika Mathayo 2:1, 11. Unaweza kuona pia kwamba Biblia haisemi kulikuwa na wanajimu wangapi.a

      Katika Amerika ya Kusini, wale wanaume watatu wenye hekima wanachukua mahali pa Baba Krismasi. Bado, kama ifanywavyo katika nchi nyingine, wazazi wengi huficha vichezeo katika nyumba. Kisha asubuhi ya Januari 6, watoto huvitafuta, kana kwamba vililetwa na wale wanaume watatu wenye hekima. Wakati huo wauza-vichezeo hupata pesa nyingi, na wengine wametajirika kutokana na jambo ambalo watu wengi wanyofu huliona kuwa fantasia tu. Watu wengi kutia ndani watoto wadogo, wanazidi kukosa imani katika ngano ya wanaume watatu wenye hekima. Ingawa wengine hawafurahii kupungua kwa watu wanaoamini ngano hiyo, mtu aweza kutarajia iweje kwa fantasia inayofuatwa tu kwa sababu ya desturi na kujinufaisha kifedha?

  • Desturi za Krismasi-Je, Ni za Kikristo?
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Desemba 15
    • Wanajimu

      Simulizi la Mathayo lataja kwamba wanajimu kutoka Mashariki walikuja Yerusalemu wakitafuta mahali alipozaliwa Mfalme wa Wayahudi. Mfalme Herode alipendezwa sana na habari hizo—lakini si kwa kusudi zuri. “Akiwatuma Bethlehemu, akasema: ‘Nendeni mkamtafute kwa uangalifu mtoto mchanga, na mkiisha kumpata leteni ripoti kwangu, ili mimi vilevile nipate kwenda na kumsujudia.’” Wanajimu walimpata huyo mtoto mchanga, “wakafungua hazina zao na kumtolea zawadi, dhahabu na ubani na manemane.” Lakini hawakurudi kwa Herode. “Walipewa onyo la kimungu katika ndoto wasirudi kwa Herode.” Mungu alitumia malaika kumwonya Yosefu kuhusu makusudio ya Herode. Ndipo Yosefu na Maria wakatorokea Misri pamoja na mwana wao. Kisha, katika jitihada ya kumwangamiza Mfalme mpya, Mfalme Herode mkatili akaagiza wavulana wauawe katika eneo la Bethlehemu. Wavulana gani? Waliokuwa na umri wa miaka miwili na walio chini ya umri huo.—Mathayo 2:1-16.

      Twaweza Kujifunza Nini Kutokana na Simulizi Hilo?

      Wanajimu waliozuru—bila kujali walikuwa wangapi—hawakuwa waabudu wa Mungu wa kweli. Tafsiri ya Biblia ya La Nueva Biblia Latinoamérica (Chapa ya 1989) yasema hivi katika kielezi-chini: “Mamajusi hao hawakuwa wafalme, bali wapiga-ramli na makuhani wa dini ya kipagani.” Walikuja kwa sababu ya ujuzi wao kuhusu nyota ambazo walikuwa wamejitoa kwake. Kama Mungu angetaka kuwaongoza hadi kwa mtoto mchanga, wangeelekezwa mahali penyewe hasa bila wao kulazimika kwenda Yerusalemu kwanza kisha kwenye jumba la mfalme Herode. Baadaye, Mungu aliingilia kati ili kugeuza safari yao kusudi amlinde mtoto huyo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki