Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuzaliwa Kunakokumbukwa
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Desemba 15
    • Mamajusi hutimiza sehemu muhimu katika Sherehe za Krismasi huko Hispania, kama vile Baba Krismasi katika nchi nyingine. Huko Hispania, inaaminika kwamba watoto hupokea zawadi zao kutoka kwa Mamajusi Januari 6, Día de Reyes (Siku ya Wafalme), kama vile Mamajusi, kulingana na maoni ya wengi, walivyoleta zawadi kwa Yesu aliyetoka kuzaliwa. Hata hivyo, ni watu wachache wanaojua kwamba masimulizi ya Injili hayataji ni Mamajusi wangapi waliomtembelea Yesu. Badala ya kuwa wafalme, wao wanajulikana kwa usahihi zaidi kuwa wanajimu.a Isitoshe, baada ya ziara ya Mamajusi, Herode aliwaua watoto wote wa kiume huko Bethlehemu “kuanzia umri wa miaka miwili kwenda chini,” akijaribu kumuua Yesu. Hilo linaonyesha kwamba ziara yao ilifanyika muda fulani baada ya kuzaliwa kwa Yesu.—Mathayo 2:11, 16.

      Tangu karne ya 12, miji fulani ya Hispania imekuwa na michezo ya kuigiza ya kuzaliwa kwa Yesu, kutia ndani ziara ya wachungaji huko Bethlehemu na baadaye ile ya Mamajusi. Siku hizi, majiji mengi ya Hispania huwa na cabalgata, au msafara kila Januari 5, ambapo “wafalme watatu” hupitishwa katikati ya mji kwa magari yaliyopambwa na ambayo yana jukwaa, huku wakiwapa watazamaji peremende. Mapambo yanayotumiwa wakati wa Krismasi na villancicos (nyimbo) hufanya sherehe hizo ziwe zenye kuchangamsha.

  • Kuzaliwa Kunakokumbukwa
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Desemba 15
    • a Kitabu La Sagrada Escritura—Texto y comentario por profesores de la Compañía de Jesús (Maandiko Matakatifu—Maandishi na Maelezo ya Maprofesa wa Shirika la Yesu) yanasema kwamba “kati ya Waajemi, Wamedi, na Wakaldayo, Mamajusi walifanyiza jamii ya ukuhani ambayo iliendeleza mambo ya uchawi, unajimu, na uganga.” Hata hivyo, kufikia Enzi za Kati, Mamajusi ambao walienda kumwona mvulana Yesu walitangazwa kuwa watakatifu na kupewa majina Melchior, Gaspar, na Balthasar. Na inadaiwa kwamba mabaki yao yamehifadhiwa katika kanisa kuu la Cologne, Ujerumani.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki