Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Latvia
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Mapema mwaka wa 1993, watafsiri walihama ile ofisi ndogo katika makao ya wamishonari huko Riga na kuingia nyumba iliyo kwenye Barabara ya Brīvības. Kisha, Agosti 1994, walihamia ofisi zilizorekebishwa kwenye Barabara ya 40 Miera. Akina ndugu walipataje ofisi hizo?

      ZAWADI

      George Hakmanis na mke wake, Sigrid, waliondoka Latvia wakiwa wakimbizi wakati wa Vita vya Pili vya Ulimwengu. Wenzi hao walijifunza kweli London, Uingereza, na kubatizwa mwaka wa 1951. Mwaka uliofuata, walihamia Marekani, na mwaka wa 1992 wakarudi Latvia kwa miaka mitano.

      Baada ya Latvia kujiondoa kwenye Muungano wa Sovieti mwaka wa 1991, watu wangeweza kudai haki ya kumiliki tena mali yao iliyochukuliwa na serikali. Kwa kuwa Sigrid na dada yake, ambaye pia ni Shahidi, walihifadhi hati za familia yao kwa miaka zaidi ya 50, walifaulu kurudishiwa mali yao iliyokuwa kwenye Barabara ya 40 Miera. Kisha, wakaitoa iwe mali ya tengenezo la Yehova. Halafu akina ndugu wakakarabati jengo lililokuwapo likawa kituo cha kutafsiri chenye orofa tano na makao ya watu 20.

      Milton G. Henschel wa Baraza Linaloongoza alihudhuria kuwekwa wakfu kwa jengo hilo mnamo Agosti 20, 1994. Alipokuwa huko, aliwashauri akina ndugu wanunue uwanja ulioko kwenye Barabara ya 42 Miera, ambao unapakana na ofisi hiyo. Uwanja huo ulikuwa na jengo la orofa sita. Mwenyewe, anayeishi Marekani, alikubali kuuza uwanja huo. Jengo hilo pia lilirekebishwa kabisa, na familia ya Betheli ikaongezeka kufikia watu 35. Tangu wakati huo, upanuzi zaidi umefanywa na sasa kuna ofisi na vyumba zaidi kwa ajili ya Wanabetheli 55.

  • Latvia
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Mwishowe, Oktoba 12, 1998, mkurugenzi wa Ofisi ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu alitangaza kwamba makutaniko mawili, yaani, Riga Center and Riga Torn̗akalns, yamesajiliwa kwa kipindi cha majaribio cha mwaka mmoja.

  • Latvia
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Wakati huohuo, ndugu katika eneo la Torn̗akalns huko Riga waliuziwa kwa bei nafuu jumba la sinema lililoungua. Kufikia Agosti 1998, jengo hilo lililokuwa limeungua lilibadilishwa kuwa Majumba mawili maridadi ya Ufalme!

  • Latvia
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • 1996 Halmashauri ya Nchi yaundwa jijini Riga.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki