Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Latvia
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • KUPATA MAHALI PA KUKUTANIA

      Kutokana na ongezeko la haraka katika miaka ya 1990, majumba makubwa zaidi yalihitajiwa kwa ajili ya mikutano. Mwaka wa 1997, jengo fulani linalofaa lilipigwa mnada huko Daugavpils, na akina ndugu tu ndio waliotaka kulinunua. Kazi ya kulirekebisha ilianza Desemba 1998, na miezi minane baadaye, wahubiri zaidi ya 140 wa jiji hilo walifurahia kukusanyika katika Jumba lao wenyewe la Ufalme.

      Jumba la Ufalme la kwanza kujengwa toka mwanzo mpaka mwisho lilikamilishwa huko Jūrmala mwaka wa 1997. Mwanafunzi mmoja wa Biblia wa eneo hilo alifurahishwa sana na ubora wa kazi iliyofanywa hivi kwamba akawaomba Mashahidi wamjengee nyumba! Akina ndugu walimwambia haitawezekana na kwamba hatufanyi biashara bali kazi yetu ni ya kidini. Wakati huohuo, ndugu katika eneo la Torn̗akalns huko Riga waliuziwa kwa bei nafuu jumba la sinema lililoungua. Kufikia Agosti 1998, jengo hilo lililokuwa limeungua lilibadilishwa kuwa Majumba mawili maridadi ya Ufalme!

  • Latvia
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • 1997 Jumba la Ufalme jipya la kwanza lajengwa Jūrmala.

  • Latvia
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 218]

      Jengo hili la sinema lililoungua (kushoto) lilirekebishwa na kuwa Majumba mawili ya Ufalme (chini)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki