Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Latvia
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Mapema mwaka wa 1927, kijana mmoja anayeitwa Ferdinand Fruck na mama yake, Emilie, walibatizwa. Miaka minne baadaye, Ferdinand alipokuwa akihubiri katika duka la kuoka mikate katika mji wa kwao wa Liepaja, alikutana na mwanamume ambaye baadaye alikuja kuwa painia mwenzake. Mwokaji huyo alienda mbio kwenye duka jirani la kinyozi aliyekuwa ndugu yake, na kumwambia, “Heinrich! Njoo haraka!” Kisha akasema: “Kuna mtu dukani kwangu ambaye anasema mambo nisiyoweza kuyaamini.” Kinyozi huyo, Heinrich Zech, hakuona vigumu kuamini kweli ya Biblia, naye akabatizwa baada ya muda mfupi. Alijiunga na Ferdinand, na wote wawili wakatembelea majiji mengi kwa baiskeli ili kueneza ujumbe wa Ufalme.

  • Latvia
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Mara nyingi, Ferdinand Fruck alikutana na akina ndugu kwenye mpaka wa Lithuania. Walimpa vichapo, naye akaviweka chini ya nyasi kavu katika dari la ghala lake. Hata hivyo, wenye mamlaka waligundua shughuli zake, na tangu wakati huo polisi wakawa wakisaka nyumba yake kutafuta vichapo vilivyopigwa marufuku. Pindi moja walipokuja kufanya msako, ofisa mmoja hakutaka kupanda katika dari la ghala, kwa hiyo akamwamuru Ferdinand apande badala yake! Ili amtulize ofisa huyo, Ferdinand alirudi na magazeti machache ya zamani ya Mnara wa Mlinzi na kumpa. Ofisa huyo akaridhika na kwenda zake.

  • Latvia
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 180]

      Ferdinand Fruck, alibatizwa 1927

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki