Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Latvia
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Utimilifu wa wengine umejaribiwa kuhusiana na suala la damu. Mnamo Septemba 6, 1996, msichana mwenye umri wa miaka 17 anayeitwa Yelena Godlevskaya aligongwa na gari na kuvunjika sehemu kadhaa za mfupa wa nyonga. Kutokana na ukomavu wake wa kiroho, Yelena aliazimia moyoni kujiepusha na damu. (Mdo. 15:29) Wakati huo, madaktari wengi nchini Latvia hawakujua mbinu za kuwatibu wagonjwa bila damu, kwa hiyo madaktari waliomshughulikia walikataa kumfanyia upasuaji. Kisha, usiku fulani karibu juma moja baadaye, madaktari wawili walimtia Yelena damu kwa lazima na kwa ukatili, naye akafa.

      Wakati huo Marina, mama ya Yelena, hakuwa Shahidi. Marina anasema: “Nilishangaa kuona jinsi binti yangu alivyomwamini sana Yehova na ahadi zake. Alikataa katakata.” Sasa Marina amebatizwa, naye na familia yake wanatazamia kumkumbatia Yelena wakati wa ufufuo.—Mdo. 24:15.

  • Latvia
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 210]

      Yelena Godlevskaya alikufa baada ya kutiwa damu mishipani kwa lazima

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki