Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Kuujua Upendo wa Kristo”
    Mkaribie Yehova
  • “Kuujua Upendo wa Kristo”
    Mkaribie Yehova
    • Kwa huruma Yesu anamgusa mwenye ukoma na kumponya

      “Akanyoosha mkono wake akamgusa”

      11, 12. (a) Wenye ukoma walitendewaje nyakati za Biblia, lakini Yesu alitendaje alipofikiwa na mtu “mwenye kujaa ukoma”? (b) Huenda mtu mwenye ukoma aliyeguswa na Yesu alihisije, na kisa halisi cha daktari mmoja kinathibitishaje jambo hilo?

      11 Alichochewa kukomesha mateso. Watu wenye magonjwa mbalimbali walivutiwa na Yesu kwa sababu walijua yeye ni mwenye huruma. Jambo hilo lilionekana wazi wakati Yesu huku akifuatwa na umati alipofikiwa na mtu “mwenye kujaa ukoma.” (Luka 5:11, 12) Katika nyakati za Biblia, wenye ukoma walitengwa ili wasiwaambukize wengine. (Hesabu 5:1-4) Lakini baada ya muda, marabi wasio na huruma walikuwa na maoni mabaya kuhusu ukoma, hivyo wakatunga sheria zao wenyewe zenye kukandamiza.a Ingawa hivyo, hebu ona jinsi Yesu alivyomtendea yule mtu mwenye ukoma: “Huko pia mwenye ukoma akaja kwake, akimsihi sana hata kwa kukunja magoti, akimwambia: ‘Ikiwa tu wewe wataka, waweza kunifanya safi.’ Ndipo akasukumwa na sikitiko, naye akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia: ‘Mimi nataka. Fanywa safi.’ Na mara hiyo ule ukoma ukamtoka.” (Marko 1:40-42) Yesu alijua kwamba mtu huyo mwenye ukoma hakupaswa kuwa miongoni mwa watu. Hata hivyo, badala ya kumfukuza, Yesu alimsikitikia sana hivi kwamba alifanya jambo la kushangaza. Yesu alimgusa!

      12 Wafikiri mtu huyo alihisije alipoguswa na Yesu? Kwa mfano, hebu fikiria kisa hiki halisi. Dakt. Paul Brand, mtaalamu wa ukoma, asimulia kuhusu mtu mmoja mwenye ukoma ambaye alimtibu nchini India. Alipokuwa akimpima, daktari huyo alimshika begani na kumweleza kupitia mkalimani matibabu ambayo angepewa. Mtu huyo alianza kulia ghafula. Daktari akamwuliza, “Nimesema jambo baya?” Mkalimani akamwuliza kijana huyo swali hilo katika lugha yake kisha akajibu: “La, daktari. Anasema analia kwa sababu umemshika begani. Hajapata kamwe kuguswa na yeyote kwa miaka mingi isipokuwa wewe.” Yule mtu mwenye ukoma aliyemfikia Yesu alifaidika hata zaidi alipoguswa naye. Baada ya kuguswa mara moja tu, ugonjwa uliomfanya atengwe na watu ulitoweka kabisa!

  • “Kuujua Upendo wa Kristo”
    Mkaribie Yehova
    • a Sheria za marabi zilisema kwamba hakuna yeyote aliyeruhusiwa kusimama umbali wa futi 6 hivi kutoka kwa mwenye ukoma. Lakini kukiwa na upepo, mwenye ukoma alisimama umbali wa futi 150 hivi. Kichapo Midrash Rabbah chataja rabi mmoja ambaye alijificha alipoona wenye ukoma, na rabi mwingine ambaye aliwatupia mawe wenye ukoma ili wasimkaribie. Kwa hiyo wenye ukoma walijua uchungu wa kukataliwa, kudharauliwa na kuchukiwa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki