-
Kuvumilia Chini ya Majaribu Humletea Yehova SifaMnara wa Mlinzi—2003 | Oktoba 1
-
-
Kwa mfano katika miaka ya 1960 Mashahidi wa Yehova walinyanyaswa kikatili nchini Malawi. Majumba yao ya Ufalme, nyumba, vyakula, na biashara zao, yaani, vitu vyote walivyokuwa navyo viliharibiwa. Walipigwa na kutendewa mambo mengine yenye kusikitisha. Ndugu hao walitendaje? Maelfu walikimbia vijiji vyao. Wengi walikimbilia msituni, huku wengine wakihamia nchi jirani ya Msumbiji kwa muda. Ingawa ndugu wengi waaminifu walikufa, wengine waliamua kukimbia eneo lenye hatari, hatua ambayo yaonekana ilifaa kuchukuliwa katika hali hizo. Kwa kufanya hivyo, ndugu hao waliiga kielelezo cha Yesu na Paulo.
6. Ni nini ambacho Mashahidi wa Malawi hawakuacha kufanya kujapokuwa mnyanyaso mkali?
6 Hata ingawa ndugu wa Malawi walilazimika kuhama au kujificha, walitafuta na kufuata mwongozo wa kiroho nao waliendelea kufanya kazi ya Kikristo kisiri kadiri walivyoweza. Ikawaje? Kulikuwa na kilele cha watangazaji wa Ufalme 18,519 kabla tu ya marufuku iliyotokea mwaka wa 1967. Kufikia mwaka wa 1972 kulikuwa na kilele kipya cha watangazaji 23,398 ingawa marufuku ilikuwa bado haijaondolewa na wengi walikuwa wamekimbilia Msumbiji. Walihubiri kwa wastani wa saa zaidi ya 16 kila mwezi. Bila shaka, walimletea Yehova sifa kwa jinsi walivyotenda, naye aliwabariki ndugu hao waaminifu wakati huo mgumu sana.a
-
-
Kuvumilia Chini ya Majaribu Humletea Yehova SifaMnara wa Mlinzi—2003 | Oktoba 1
-
-
a Matukio ya miaka ya 1960 yalikuwa mwanzo tu wa mfululizo wa mnyanyaso wa kikatili ambao ungewapata Mashahidi nchini Malawi kwa miaka karibu thelathini. Kwa habari kamili, ona kitabu 1999 Yearbook of Jehovah’s Witnesses, ukurasa wa 171-212.
-