-
Kuja kwa Yesu au Kuwapo kwa Yesu—ni Kupi?Mnara wa Mlinzi—1996 | Agosti 15
-
-
Twaona jambo hilo kutoka katika kile kitabu cha 1995 cha Hebrew Gospel of Matthew, cha Professor George Howard. Kitabu hicho kilikazia maandishi fulani yenye ubishi dhidi ya Ukristo ya karne ya 14 yaliyoandikwa na tabibu Myahudi Shem-Tob ben Isaac Ibn Shaprut. Hati hiyo ilikuwa na maandishi ya Kiebrania ya Gospeli ya Mathayo. Kuna uthibitisho kwamba badala ya kutafsiriwa kutoka Kilatini au Kigiriki katika wakati wa Shem-Tob, maandishi hayo ya Mathayo yalikuwa mazee sana na awali yalikuwa yametungwa katika Kiebrania.c Kwa njia hiyo hayo yaweza kutuleta karibu zaidi na yale yaliyosemwa kwenye Mlima wa Mizeituni.
-
-
Kuja kwa Yesu au Kuwapo kwa Yesu—ni Kupi?Mnara wa Mlinzi—1996 | Agosti 15
-
-
c Uthibitisho mmoja ni kwamba mara 19, yana ule usemi wa Kiebrania “Lile Jina,” ukiwa umeandikwa mzima au kwa ufupi. Profesa Howard aandika hivi: “Kusoma Jina la Kimungu katika hati ya Kikristo iliyonukuliwa na mwandishi Myahudi wa makala zenye ubishi ni jambo la kutokeza. Ikiwa hii ingekuwa tafsiri ya Kiebrania ya hati ya Kikristo ya Kigiriki au ya Kilatini, mtu angetazamia kupata adonai [Bwana] katika maandishi, si ufananisho wa lile jina tukufu la kimungu YHWH. . . . Jambo la kwamba aliongeza jina hilo tukufu halielezeki. Uthibitisho hudokeza kwa nguvu kwamba Shem-Tob alipokea nakala yake ya Mathayo ikiwa tayari na Jina la Kimungu katika maandishi na kwamba labda alilihifadhi badala ya kujasiri kuwa na hatia ya kuliondoa.” Biblia ya New World Translation of the Holy Scriptures—With References hutumia maandishi ya Mathayo (J2) ya Shem-Tob kuwa utegemezo wa kutumia jina la kimungu katika Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo.
-