Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Melkizedeki—Alikuwa Nani?
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Februari 15
    • Cheo cha kikuhani cha Melkizedeki hakikuhusiana na ukuhani wa Israeli, na kama vile Maandiko yanavyoonyesha, kilikuwa bora kuliko ukuhani wa Aroni. Jambo moja linaloonyesha hivyo ni jinsi ambavyo Abrahamu, yule baba wa zamani wa taifa lote la Israeli, na wa kabila la kikuhani la Lawi alivyomstahi Melkizedeki. Abrahamu, “rafiki ya Yehova,” aliyekuwa “baba ya wote wale walio na imani,” alimtolea huyo kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana “sehemu ya kumi.” (Yakobo 2:23; Waroma 4:11) Paulo aonyesha kwamba Walawi walikusanya sehemu ya kumi kutoka kwa ndugu zao, ambao pia walitoka katika viuno vya Abrahamu. Hata hivyo, Paulo aeleza kwamba Melkizedeki “ambaye hakufuatisha nasaba yake kutoka kwao alichukua sehemu za kumi kutoka kwa Abrahamu,” na “kupitia Abrahamu hata Lawi ambaye hupokea sehemu za kumi amelipa sehemu za kumi, kwa maana alikuwa bado katika viuno vya baba yake wa zamani wakati Melkizedeki alipokutana naye.” Hivyo basi, ingawa makuhani Walawi walipokea sehemu za kumi kutoka kwa Waisraeli, wao, kama wawakilishwavyo na mzazi wao wa kale Abrahamu, walimpa Melkizedeki sehemu za kumi. Zaidi ya hilo, ubora wa ukuhani wa Melkizedeki waonyeshwa na jambo la kwamba yeye alimbariki Abrahamu, Paulo akionyesha kwamba ‘mdogo hubarikiwa na mkubwa zaidi.’ Hizo ni baadhi ya zile sababu zinazomfanya Melkizedeki awe ufananisho unaofaa wa Kuhani wa Cheo cha Juu aliye mkuu Yesu Kristo.—Waebrania 7:4-10.

  • Melkizedeki—Alikuwa Nani?
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Februari 15
    • Ndipo Abrahamu akampa mfalme huyo aliyekuwa kuhani “fungu la kumi la vitu vyote,” yaani “nyara zilizo kuu” alizozitwaa katika ushindi wake kwenye vita dhidi ya wale wafalme walioungana.—Mwanzo 14:17-20; Waebrania 7:4.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki