Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kucheza Dansi Pamoja na Korongo
    Amkeni!—2003 | Septemba 22
    • Safari za Korongo

      Mara nyingi unaweza kuwasikia korongo kabla hujawaona. Unaweza kusikia mlio wao mrefu kama wa tarumbeta, hata ingawa huenda wakawa mbali sana. Yaelekea mlio huo huwasaidia kuambatana katika safari zao ndefu za kuhama. Aina nyingi za korongo huhama maeneo ya kaskazini ya kuzalia. Kabla ya majira ya baridi kali kuanza huko Kanada, Skandinavia, au Siberia wao husafiri mwendo mrefu sana hadi sehemu za joto za China, India, Marekani (Texas), au eneo la Mediterania. Safari hizo za korongo ni hatari na zenye kuchosha. Korongo fulani wanaotoka Ulaya na Asia wameonekana wakiruka kwenye mwinuko wa meta 10,000 hivi walipokuwa wakivuka milima ya Himalaya wakielekea India. Korongo huruka wakiwa wamejipanga kwa muundo wa herufi ya V na wakifikia hewa yenye joto wao hutumia nafasi hiyo kunyiririka mbali iwezekanavyo bila kutumia mabawa. Hata hivyo, wanapovuka bahari na maziwa ni lazima watumie mabawa.a

      Kwa miaka 20 hivi, Juan Carlos Alonso, mtaalamu wa ndege Mhispania, amechunguza safari za wale korongo 70,000 wa Asia na Ulaya wanaohamia Hispania kila mwaka. Anasema hivi: ‘Baadhi ya ndege hutiwa alama mguuni na wengine wanawekwa vifaa vya kupokea na kupasha habari ili tujue mahali walipo wanaposafiri. Mimi husisimuka sana ninapomwona ndege huku Hispania, niliyemtia alama mguuni huko Ujerumani Kaskazini alipokuwa mdogo. Kwa mamia ya miaka, korongo wamepitia sehemu zilezile wanapohama. Mmoja aliyetiwa alama nchini Ufini, alipatikana Ethiopia, na baadhi ya korongo kutoka Siberia huhamia Mexico.’

  • Kucheza Dansi Pamoja na Korongo
    Amkeni!—2003 | Septemba 22
    • a Maelfu ya korongo kutoka Asia na Ulaya hupita nchi ya Israel wanapohama kabla ya majira ya baridi kali kuanza katika maeneo yao ya kuzalia na wanaporudi kwenye maeneo hayo. Wengine wao pia huhamia nchi hiyo. Jioni-jioni katika sehemu ya kaskazini ya Bonde la Yordani, watu wanaweza kuona vikundi vya korongo wakipita Mlima Hermoni uliofunikwa kwa theluji. Lakini mandhari hiyo yenye kuvutia huonekana kwa muda mfupi tu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki