Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Matukio Muhimu ya Mwaka Uliopita
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Jumamosi, Mei 8, 2010, zaidi ya watu 2,200 walifurahia hotuba ya kuwekwa wakfu iliyotolewa katika ofisi ya tawi ya Paraguai na Gerrit Lösch wa Baraza Linaloongoza. Nyumba ya makazi yenye vyumba 32 na jengo jipya lenye ofisi lilijengwa, na majengo ya makazi yaliyokuwepo yalirekebishwa na kujengwa upya. Zaidi ya hilo, tangi la maji linaloweza kubeba maji ya lita 40,000 lilijengwa. Tangu mwanzo, wenye mamlaka wa eneo hilo wamefurahishwa sana na ubora wa kazi ambayo imefanywa na wajitoleaji wa kimataifa na wa eneo hilo. Ofisa mmoja alisema kwamba majengo mengine ya kidini yamekuwa na matatizo mengi lakini Mashahidi wa Yehova walikuwa na sifa ya kufanya kila kitu kwa usahihi. Kwa sababu hiyo, ilikuwa rahisi sana kupata vibali vya ujenzi kwa ajili ya ofisi ya tawi.

  • Matukio Muhimu ya Mwaka Uliopita
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 37]

      Ofisi ya tawi ya Paraguai

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki