Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 2/22 kur. 22-23
  • Neem Wenye Kushangaza

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Neem Wenye Kushangaza
  • Amkeni!—1998
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Fungu Lake Ukiwa Mti
  • Wadudu Huuchukia
  • “Duka la Dawa la Kijiji”
  • Kijiti cha Kusugua Meno
    Amkeni!—2003
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2005
  • Kuzuia “Busu” la Kifo
    Amkeni!—2000
  • “Mti wa Uhai” Wenye Kushangaza wa Afrika
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 2/22 kur. 22-23

Neem Wenye Kushangaza

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA NIGERIA

“DUKA la dawa la kijiji”—hivyo ndivyo watu huuita mti wa neem katika India. Kwa karne kadhaa watu katika nchi hiyo wameutegemea mti wa neem ili kutoa kitulizo kwa maumivu, homa, na maambukizo. Wakiamini kuwa neem waweza kusaidia kuisafisha damu yao, Wahindi wengi huanza kila mwaka kwa kula matawi machache ya neem. Watu pia husafisha meno yao kwa kutumia vijiti vya neem, wanapaka umajimaji wa matawi ya neem kwenye miparaganyo ya ngozi, na kunywa chai ya neem kama dawa ya kuchangamsha mwili.

Katika miaka ya karibuni wanasayansi wameonyesha upendezi mwingi kuelekea neem. Hata hivyo, ripoti ya kisayansi yenye kichwa Neem—A Tree for Solving Global Problems yaonya: “Ijapokuwa uwezekano waelekea kuwa usio na mwisho, hakuna jambo lolote kuhusu neem lililo dhahiri. Wanasayansi walio na shauku kuelekea mmea huo na yanayotazamiwa kuwa matokeo wanakiri kwamba katika wakati huu uthibitisho wa kutetea matazamio yao si hakika.” Hata hivyo, ripoti hiyo pia yataarifu hivi: “Miongo miwili ya utafiti imetokeza matokeo yenye ahadi katika nyanja nyingi sana za mafunzo ambazo neem waweza kuwa wa manufaa mengi kwa nchi maskini na tajiri pia. Hata baadhi ya watafiti walio na tahadhari zaidi wanasema kuwa ‘neem wastahili kuitwa mti wa ajabu.’”

Fungu Lake Ukiwa Mti

Neem hupatikana katika maeneo ya kitropiki ukiwa mshiriki wa familia ya miti ya mkangazi. Humea kufikia urefu wa meta 30 na waweza kupata upana wa zaidi ya meta 2.5. Kwa kuwa ni nadra kuwa hauna matawi, huo huandaa kivuli muda wote wa mwaka. Hukua haraka, huhitaji utunzaji mdogo, na hufanya vizuri katika udongo usio mzuri.

Uliletwa katika Afrika Magharibi mapema katika karne hii ili kutoa kivuli na kukomesha kusonga kuelekea kusini mwa Jangwa la Sahara. Wanamisitu pia wameusitawisha mti huu katika Fiji, Mauritius, Saudi Arabia, na Amerika ya Kati na Kusini, na visiwa vya Karibea. Katika Marekani kuna viwanja vya kufanyia majaribio kutia sehemu za kusini mwa Arizona, California, na Florida.

Kwa kuongezea kutoa kivuli kwa muda wote wa mwaka katika sehemu zenye tabia ya nchi yenye joto, neem waweza kutumika kwa kuni. Zaidi ya hayo, mbao zake zenye kukinza mchwa ni zenye mafaa katika ujenzi na useremala. Kwa hiyo, kwa kuamua tu kwa kutegemea msingi wa kuwa wenye mafaa ukiwa mti, neem ni wenye matumizi mengi sana. Lakini huo ni mwanzo tu.

Wadudu Huuchukia

Kwa sababu watu wa India kwa muda mrefu wamejua kuwa majani ya neem huwafukuzia mbali wadudu wasumbufu, wao huweka majani ya neem kwenye vitanda, vitabu, mapipa, kabati, na kabati za nguo. Katika 1959 Mjerumani aliyekuwa bingwa wa elimu ya wadudu pamoja na wanafunzi wake walihusika katika utafiti kuhusu neem baada ya kushuhudia pigo kubwa sana la nzige katika Sudan ambalo mabilioni ya nzige walimeza matawi ya kila mti isipokuwa neem.

Tangu wakati huo, wanasayansi wamejifunza kuwa akiba ya dawa ya neem iliyo tata ni yenye matokeo dhidi ya spishi zaidi ya 200 za wadudu vilevile na baadhi ya wadudu wadogo waharibifu, nematodi, fuvu, bakteria, na hata baadhi ya virusi. Katika jaribio moja, watafiti waliweka majani ya soya katika kiwekeo pamoja na kombamwiko wa Japani. Nusu ya kila jani ilikuwa imepuliziwa umajimaji wa neem. Kombamwiko hao walimeza sehemu ambazo hazikuwa na umajimaji huo lakini zilizokuwa nao hata hawakuzigusa. Kwa hakika, walikufa njaa badala ya kula hata sehemu ndogondogo za majani hayo yaliyopuliziwa.

Majaribio kama hayo yanadokeza uwezekano wa kutokeza kibadala cha viua-wadudu sanisia fulani, kisicho ghali, kisicho na sumu kwa wanadamu, wanyama, au ndege na rahisi kutengeneza. Kwa kielelezo katika Nikaragua, wakulima huchanganya mbegu za neem zilizosagwa pamoja na maji—gramu 80 za mbegu kwa kila lita moja ya maji. Wanaloweka mbegu hizo zilizopondwa kwa muda wa saa 12, wanaondoa mbegu hizo, kisha wananyunyizia maji hayo kwa mimea.

Bidhaa za neem haziui wadudu wengi papo hapo. Minyunyizo ya neem hubadili mwendo wa maisha ya mdudu, ili kwamba hatimaye, hataweza kula, kuzaana, au kubadilika. Lakini ingawa bidhaa za neem huwadhuru wadudu, hazielekei kuwa zenye madhara kwa ndege, wanyama wenye damu moto, au wanadamu.

“Duka la Dawa la Kijiji”

Kisha kuna manufaa nyingine kwa wanadamu. Mbegu na matawi huwa na michanganyiko ambayo hutokeza sifa za kuwa antiseptiki, kizuia-virusi, na kizuia-kuvu. Kuna madokezo kwamba neem waweza kupigana dhidi ya uvimbeuchungu, mpigo mkubwa wa moyo, na vidonda vya tumbo. Dawa kutoka kwa umajimaji wa neem husemekana kuwa hupigana na ugonjwa wa kisukari na malaria. Faida nyingine zitarajiwazo zatia ndani:

Vifukuza-wadudu. Mchanganyiko mmoja wa neem, uitwao salannin, hufukuza kwa nguvu aina fulani ya wadudu wenye kuuma. Kifukuza-nzi na kifukuza-mbu kilichotengenezwa kutokana na mafuta ya neem tayari chauzwa madukani.

Usafi wa kiafya wa meno. Mamilioni ya Wahindi huvunja kijiti cha neem kila asubuhi, wanatafuna mwisho ili kuufanya uwe mwororo, kisha wanakitumia kusugua meno yao na ufizi. Utafiti waonyesha kuwa hili ni lenye manufaa, kwani michanganyiko katika ganda huwa ni antiseptiki yenye nguvu.

Sifa za kuwa kizuia-mimba. Mafuta ya neem ni dawa ya kuua shahawa yenye nguvu na imethibitika kuwa na matokeo katika kupunguza kiwango cha uzalishaji kati ya wanyama wa maabara. Majaribio yaliyofanyiwa tumbili yadokeza kwamba mchanganyiko wa neem waweza pia kufanya iwezekane kuwe na tembe za kudhibiti uzazi kwa wanaume.

Waziwazi, neem si mti wa kawaida. Ijapokuwa hakuna uthibitisho kamili, neem huonyesha matumaini makubwa—kuboresha udhibiti wa wadudu, kuendeleza afya, kusaidia katika kurudisha misitu, na, labda, kuzuia kuongezeka mno kwa idadi ya watu. Haishangazi kwamba watu wameuita neem wenye kustaajabisha “zawadi kutoka kwa Mungu kwa wanadamu”!

[Picha katika ukurasa wa 23]

“Neem,” na picha ndogo ya jani la “neem”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki