Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 4. (a) Ni katika njia zipi Israeli wa kale alifanya uasherati? (b) Ni katika njia gani ya kutokeza Babuloni Mkubwa amefanya uasherati?

      4 Babuloni (au Babeli, kumaanisha “Mvurugo”) lilifikia kilele chalo cha ukubwa wakati wa Nebukadneza. Lilikuwa dola la dini-siasa lenye mahekalu na vikanisa zaidi ya elfu moja. Ukuhani walo ulitumia nguvu kubwa. Ingawa muda mrefu tangu hapo Babuloni limeacha kuwa serikali ya ulimwengu, Babuloni Mkubwa wa kidini huendelea kuwapo, na kwa kufuata kigezo cha kale, yeye angali anatafuta kuvuta na kuunda mambo ya kisiasa. Lakini je! Mungu anatoa idhini ya dini kuwa katika siasa? Katika Maandiko ya Kiebrania, Israeli alisemwa kuwa alifanya ukahaba wakati alipojihusisha katika ibada bandia na wakati badala ya kuitibari katika Yehova, alifanya mafungamano na mataifa. (Yeremia 3:6, 8, 9; Ezekieli 16:28-30) Babuloni Mkubwa pia hufanya uasherati. Kwa kutokeza, yeye amefanya lolote analoona linafaa ili kupata uvutano na mamlaka juu ya wafalme wa dunia wenye kutawala.—1 Timotheo 4:1.

      5. (a) Viongozi wa kidini hufurahia umashuhuri gani? (b) Kwa nini kutamani umashuhuri wa kilimwengu kunapingana moja kwa moja na maneno ya Yesu Kristo?

      5 Leo, mara nyingi viongozi wa kidini hugombea cheo cha juu katika serikali, na katika mabara fulani, wanashiriki katika serikali, hata wakishikilia vyeo katika bunge. Katika 1988 viongozi wa kidini wa Kiprotestanti wawili wenye kujulikana sana waligombea cheo cha rais wa United States. Viongozi katika Babuloni Mkubwa hupenda umashuhuri; foto zao mara nyingi zitaonekana katika nyusipepa za umma wanapofuatana na wanasiasa mashuhuri. Kwa kutofautiana, Yesu aliepuka kujihusisha katika siasa na akasema hivi kwa habari ya wanafunzi wake: “Wao si sehemu ya ulimwengu, kama vile mimi si sehemu ya ulimwengu.”—Yohana 6:15; 17:16, NW; Mathayo 4:8-10; ona pia Yakobo 4:4.

      ‘Ukahaba’ wa Ki-Siku-Hizi

      6, 7. (a) Chama cha Nazi cha Hitla kilipataje mamlaka katika Ujeremani? (b) Itifaki ambayo Vatikani ilifanya pamoja na Ujeremani ya Nazi ilisaidiaje Hitla katika jitihada yake kubwa ya kutawala ulimwengu?

      6 Kupitia udukizi wake katika siasa, huyu kahaba mkubwa ameletea aina ya binadamu huzuni isiyoelezeka. Mathalani, fikiria mambo ya hakika yaliyomwezesha Hitla kuinuka kwenye mamlaka katika Ujeremani—mambo ya hakika yenye kuchukiza sana ambayo baadhi ya watu wangependa kuyafuta kutoka katika vitabu vya historia. Katika Mei 1924 Chama cha Nazi kilishikilia viti 32 katika Bunge la Ujeremani. Kufikia Mei 1928 vilikuwa vimepungua vikawa viti 12. Lakini, ule Mshuko Mkubwa wa Thamani ya Pesa ukagharikisha ulimwengu katika 1930; kufuata huo, Wanazi walipata nafuu yenye kutokeza, wakijipatia viti 230 kati ya 608 katika machaguzi ya Ujeremani ya Julai 1932. Hivyo, wakawa chama kikubwa zaidi ya vyote katika Bunge. Upesi baadaye, Franz von Papen, Mheshimiwa Kipapa, aliyekuwa Chansela hapo kwanza, akaja kusaidia Wanazi. Kulingana na wanahistoria, von Papen alikuwa na njozi ya Milki Takatifu ya Kiroma mpya. Muda wake mwenyewe mfupi wa kuwa Chansela ulikuwa umekuwa usiofanikiwa, hivyo sasa yeye alitumainia kujipatia mamlaka kupitia Wanazi. Kufikia Januari 1933, yeye alikuwa amepata uungaji-mkono kwa ajili ya Hitla kutoka kwa wenye viwanda, na kwa njama za hila yeye alihakikisha kwamba Hitla amekuwa Chansela wa Ujeremani katika Januari 30, 1933. Yeye mwenyewe alifanywa makamu wa Chansela na yeye alitumiwa na Hitla apate uungaji-mkono wa sehemu za Kikatoliki za Ujeremani. Kwa muda wa miezi miwili ya kujipatia mamlaka, Hitla alivunja bunge, akapeleka maelfu ya viongozi wapinzani kwenye kambi za mateso, na akaanza kampeni iliyo wazi ya kuwaonea Wayahudi.

      7 Katika Julai 20, 1933, upendezi wa Vatikani katika mamlaka iliyokuwa ikiinuka ya Unazi ulionyeshwa wakati Kardinali Pacelli (ambaye baadaye akawa Papa Pius 12) alipotia sahihi itifaki katika Roma kati ya Vatikani na Ujeremani ya Nazi. Von Papen alitia sahihi hati hiyo akiwa mwakilishi wa Hitla, na huko huko Pacelli akampa von Papen medali ya juu ya kipapa ya Msalaba Mtukufu wa Daraja la Pius.b Katika kitabu chake Satan in Top Hat, Tibor Koeves huandika juu ya hili, akitaarifu: “Itifaki ilikuwa ushindi mkubwa kwa ajili ya Hitla. Ilimpa uungaji-mkono wa kwanza wa kiadili aliokuwa amepokea kutoka ulimwengu wa nje, na huo kutoka chimbuko lililokwezwa zaidi sana.” Itifaki hiyo ilitaka Vatikani iondoe uungaji-mkono wayo kutoka kwa Chama cha Kati cha Kikatoliki, na hivyo kuidhinisha “serikali jumla” ya Hitla ya chama kimoja.c Zaidi, sehemu ya 14 yayo ilisema: “Uwekwaji rasmi wa maaskofu wakuu, maaskofu, na wengine kama hao utatolewa baada tu ya gavana, aliyewekwa na Serikali, kuhakikisha kabisa kwamba hakuna shaka lolote kwa habari ya mafikirio ya ujumla ya kisiasa.” Kufikia mwisho wa 1933 (uliotangazwa na Papa Pius 11 kuwa “Mwaka Mtakatifu”), uungaji-mkono wa Vatikani ulikuwa umekuwa umechangia sana jitihada kubwa ya Hitla kwa ajili ya utawala wa ulimwengu.

      8, 9. (a) Vatikani na pia Kanisa Katoliki na viongozi wa kidini wayo walitendaje katika kuitikia ukatili wa Nazi? (b) Ni taarifa gani ambayo Maaskofu Wakatoliki wa Ujeremani walitoa mwanzoni mwa Vita ya Ulimwengu 2? (c) Mahusiano ya dini-siasa yamekuwa na matokeo gani?

      8 Ingawa mapadri na watawa wa kike wachache waliteta dhidi ya matendo ya ubahaimu ya Hitla—na wakapata mateso kwa kufanya hivyo—Vatikani pamoja na Kanisa Katoliki na jeshi layo la viongozi wa kidini waliunga mkono ukatili wa Nazi ama kwa vitendo au kwa kutoteta, waliuona kuwa kinga dhidi ya kusonga mbele kwa Ukomunisti wa ulimwengu. Akijikalia kitako katika Vatikani, Papa Pius 12 aliachilia Uharibifu Mkubwa wa Wayahudi na unyanyaso wa ukatili juu ya Mashahidi wa Yehova na wengine uendelee bila kuchambuliwa. Ni kinyume kwamba Papa John Paul 2, alipozuru Ujeremani katika Mei 1987, alipaswa kutukuza msimamo wa padri mmoja mwenye moyo mweupe wa kupinga Unazi. Yale maelfu mengine ya viongozi wa kidini wa Ujeremani walikuwa wakifanya nini wakati wa utawala wa kuogofya wa Hitla? Barua moja ya uchungaji iliyotolewa na maaskofu wa Ukatoliki wa Ujeremani katika Septemba 1939 ilipotokea Vita ya Ulimwengu 2, inatoa nuru juu ya jambo hili. Kwa sehemu inasomwa hivi: “Katika saa hii ya kukata maneno sisi twashauri askari-jeshi Wakatoliki kufanya wajibu wao katika utii kwa Fuehrer na kuwa tayari kudhabihu nafsi nzima yao. Sisi tunasihi Waaminifu wajiunge katika sala zenye idili kwamba huu Mwongozo wa Kimungu uweze kupeleka vita hii kwenye ufanisi wenye baraka.”

      9 Ubalozi huu wa Katoliki unatoa kielezi cha namna ya ukahaba ambao dini imejitia ndani yao katika miaka zaidi ya 4,000 iliyopita katika kubembeleza Serikali ya kisiasa ili kupata mamlaka na faida. Mahusiano kama hayo ya dini-siasa yamesitawisha vita, minyanyaso, na taabu kwa aina ya binadamu kwa kadiri kubwa mno. Jinsi aina ya binadamu inavyoweza kuwa na furaha kwamba hukumu ya Yehova juu ya huyu kahaba mkubwa imekaribia karibu! Na itekelezwe upesi!

      Kuketi Juu ya Maji Mengi

      10. Ni “maji mengi” gani ambayo Babuloni Mkubwa hutegemea kuwa himaya, na yanapatwa na nini?

      10 Babuloni wa kale aliketi juu ya maji mengi—Mto Eufrati na mifereji mingi. Haya yalikuwa himaya yake pamoja na chimbuko la biashara iliyotokeza utajiri, mpaka yalipokaushwa usiku mmoja. (Yeremia 50:38; 51:9, 12, 13) Babuloni Mkubwa pia hutegemea “maji mengi” yampe himaya na kumtajirisha. Maji haya ya ufananisho ni “vikundi vya watu na umati wa watu na mataifa na ndimi,” yaani, maelfu ya mamilioni yote ya binadamu ambao juu yao yeye ametawala na ambao kutoka kwao yeye amechota msaada wa vitu vya kimwili. Lakini maji haya ya ufananisho yanakauka pia, au kuondoa msaada.—Ufunuo 17:15, NW; linga Zaburi 18:4; Isaya 8:7.

      11. (a) Jinsi gani Babuloni wa kale ‘alifanya dunia yote ilewe’? (b) Babuloni Mkubwa ‘amefanyaje dunia yote ilewe’?

      11 Na zaidi, Babuloni wa kale alielezwa kuwa “kikombe cha dhahabu katika mkono wa Yehova, akifanya dunia yote ilewe.” (Yeremia 51:7, NW) Babuloni wa kale alilazimisha mataifa jirani kumeza maonyesho ya kasirani ya Yehova alipoyashinda kijeshi, kuyafanya dhaifu kama wanadamu waliolewa. Katika njia hiyo, alikuwa chombo cha Yehova. Babuloni Mkubwa, pia, amefanya ushindi mwingi kwa kadiri ya kuwa milki ya ulimwenguni pote. Lakini yeye kwa uhakika si chombo cha Yehova. Badala ya hivyo, yeye ametumikia “wafalme wa dunia” ambao pamoja nao yeye hufanya uasherati wa kidini. Yeye hufurahisha wafalme hawa kwa kutumia mafundisho yake ya uwongo na mazoea yenye kutumikisha ili kuweka matungamo ya watu, “wale wanaoikaa dunia,” kuwa dhaifu kama wanadamu waliolewa, wakitii watawala wao bila kuwa na la kufanya.

      12. (a) Kisehemu kimoja cha Babuloni Mkubwa katika Japani kilikuwaje na daraka la kumwagwa kwa damu nyingi wakati wa Vita ya Ulimwengu 2? (b) Jinsi gani “maji” yenye kuunga mkono Babuloni Mkubwa yaliondolewa katika Japani, na kukiwa na tokeo gani?

      12 Japani ya Shinto hutoa kielelezo kinachostahili kuangaliwa cha jambo hili. Askari-jeshi Wajapani waliiona kuwa heshima ya juu zaidi sana kutoa uhai wao kwa ajili ya maliki—mungu mkuu wa Shinto. Wakati wa Vita ya Ulimwengu 2, askari-jeshi Wajapani wapatao 1,500,000 walikufa vitani; karibu kila mtu aliona kusalimu amri kuwa utovu wa heshima. Lakini likiwa tokeo la ushinde wa Japani, Maliki Hirohito alilazimika kukana dai lake la uungu. Hilo lilitokeza mwondoleo mkubwa wa “maji” yaliyounga mkono kisehemu cha Shinto cha Babuloni Mkubwa—loo! baada ya Ushinto kuidhinisha umwagaji wa ndoo nyingi za damu katika uwanja wa vita wa Pasifiki! Mdhoofisho huu wa uvutano wa Shinto ulifungua pia njia katika miaka ya juzi kwa ajili ya Wajapani 200,000, ambao walio wengi wao walikuwa hapo kwanza Washinto na Wabuddha, wawe wahudumu walio wakfu na waliobatizwa wa Yehova Bwana Mwenye Enzi Kuu.

      Kahaba Apanda Hayawani

      13. Ni mwono gani wenye kushangaza anaoona Yohana wakati malaika anapompeleka katika jangwa kwa nguvu ya roho?

      13 Unabii hufumbua nini zaidi kwa habari ya kahaba mkubwa na msiba wake? Kama Yohana anavyosimulia sasa, mandhari nyingine iliyo wazi sana yaonekana: “Na yeye [malaika] akapeleka mimi mbali kwa nguvu ya roho kuingia ndani ya jangwa. Na mimi nikaona mwanamke akiwa ameketi juu ya hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu ambaye alikuwa amejaa majina ya kufuru na ambaye alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.”—Ufunuo 17:3, NW.

      14. Ni kwa nini inafaa kwamba Yohana alipelekwa jangwani?

      14 Ni kwa nini Yohana anapelekwa ndani ya jangwa? Tamko la mapema zaidi la uangamivu dhidi ya Babuloni wa kale lilielezwa kuwa “dhidi ya jangwa la bahari.” (Isaya 21:1, 9, NW) Hilo lilitoa onyo linalostahili kwamba, ujapokuwa ulinzi wake mwingi wa kimaji, Babuloni wa kale angekuwa ukiwa usio na uhai. Inafaa, basi, kwamba yampasa Yohana apelekwe katika njozi yake kwenye jangwa akaone msiba wa Babuloni Mkubwa. Yeye pia lazima awe ukiwa na utupu. (Ufunuo 18:19, 22, 23) Ingawa hivyo, Yohana anashangazwa na anachoona nje kule. Kahaba mkubwa hayuko peke yake! Yeye anaketi juu ya dubwana la hayawani-mwitu!

      15. Ziko tofauti gani kati ya hayawani-mwitu wa Ufunuo 13:1 na yule wa Ufunuo 17:3?

      15 Hayawani-mwitu huyu ana vichwa saba na pembe kumi. Basi, je! yeye ni hayawani-mwitu yule yule ambaye Yohana aliona mapema zaidi, ambaye pia alikuwa na vichwa saba na pembe kumi? (Ufunuo 13:1) La, ziko tofauti. Hayawani-mwitu huyu ni rangi-nyekundu-nyangavu na, tofauti na hayawani-mwitu aliyetangulia, hasemwi kuwa ana mataji. Badala ya yeye kuwa na majina ya kufuru juu ya vichwa vyake saba tu, yeye ‘anajaa majina ya kufuru.’ Hata hivyo, lazima pawe na uhusiano kati ya hayawani-mwitu mpya na yule aliyetangulia; mifanano kati yao ni mingi mno kuwa ya nasibu.

      16. Ni nini utambulisho wa huyo hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu, na imetaarifiwa nini kwa habari ya kusudi lake?

      16 Basi, hayawani-mwitu mpya rangi-nyekundu-nyangavu ni nini? Yeye ni lazima awe ule mfano wa hayawani-mwitu ambao ulitokezwa kwa himizo la hayawani-mwitu Uingereza-Amerika aliyekuwa na pembe mbili mithili ya mwana-kondoo. Baada ya mfano huo kuwa umefanywa, huyo hayawani-mwitu mwenye pembe mbili aliruhusiwa kuupa pumzi huo mfano wa hayawani-mwitu. (Ufunuo 13:14, 15) Yohana anaona sasa mfano ulio hai, unaopumua. Ni picha ya tengenezo la Ushirika wa Mataifa ambalo hayawani-mwitu mwenye pembe mbili alileta kwenye uhai katika 1920. Rais Wilson wa U.S. alikuwa na njozi ya kwamba Ushirika huo “ungekuwa baraza la kutolea watu wote haki na kufutilia mbali milele tisho la vita.” Lilipofufuliwa baada ya vita ya ulimwengu ya pili likiwa Umoja wa Mataifa, kusudi la katiba yalo lilikuwa “kudumisha amani na usalama wa kimataifa.”

      17. (a) Ni katika njia gani huyo hayawani-mwitu wa ufananisho rangi-nyekundu-nyangavu anajaa majina ya kufuru? (b) Ni nani anayempanda huyo hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu? (c) Dini ya Kibabuloni ilijifungamanishaje na Ushirika wa Mataifa na mwandamizi wao pale pale mwanzoni?

      17 Ni katika njia gani huyu hayawani-mwitu wa ufananisho anajaa majina ya kufuru? Katika njia ya kwamba wanadamu wameisimamisha sanamu hii ya kuabudiwa na mataifa mengi ikiwa kibadala cha Ufalme wa Mungu—itimize jambo ambalo Mungu husema ni Ufalme wake pekee unaoweza kutimiza. (Danieli 2:44; Mathayo 12:18, 21) Ingawa hivyo, jambo lenye kutokeza kuhusu njozi ya Yohana ni kwamba, Babuloni Mkubwa anapanda hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu. Kupatana na ukweli wa unabii, dini ya Kibabuloni, hasa katika Jumuiya ya Wakristo, imejifungamanisha yenyewe na Ushirika wa Mataifa na mwandamizi wao. Mapema kama Desemba 18, 1918, shirika ambalo sasa linajulikana kuwa Baraza la Taifa la Makanisa ya Kristo katika Amerika lilipitisha julisho-wazi lililojulisha wazi kwa sehemu hivi: “Ushirika kama huo si manufaa ya kisiasa tu; badala ya hivyo ni wonyesho wa kisiasa wa Ufalme wa Mungu duniani. . . . Kanisa linaweza kutoa roho ya nia njema, ambayo bila hiyo hakuna Ushirika wa Mataifa unaoweza kudumu. . . . Ushirika wa Mataifa una mizizi katika Gospeli. Kama Gospeli, lengo lao ni ‘amani duniani, nia njema kuelekea wanadamu.’”

      18. Viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo walionyeshaje uungaji-mkono wao kwa Ushirika wa Mataifa?

      18 Katika Januari 2, 1919, San Fransisco Chronicle lilikuwa na kichwa kikuu cha habari kwenye ukurasa wa kwanza: “Papa Asihi Ukubaliwe Ushirika wa Maitafa wa Wilson.” Katika Oktoba 16, 1919, ombi rasmi lililotiwa sahihi na makasisi wa vikundi mashuhuri 14,450 lilitolewa kwenye Seneti ya U.S., kuhimiza baraza hilo ‘liidhinishe mwafaka wa amani wa Paris uliotia ndani agano la ushirika wa mataifa.’ Ingawa Seneti ya U.S. ilishindwa kuidhinisha mwafaka huo, viongozi wa Jumuiya ya Wakristo waliendelea kufanya kampeni kwa ajili ya huo Ushirika. Na Ushirika huo ulizinduliwaje? Habari iliyopelekwa kutoka Uswisi, yenye tarehe ya Novemba 15, 1920, ilisomwa hivi: “Kufunguliwa kwa kusanyiko la kwanza la Ushirika wa Mataifa kulitangazwa kwenye saa tano asubuhi hii kwa kupigwa kengele zote za kanisa katika Geneva.”

      19. Wakati hayawani-mwitu alipotokea, jamii ya Yohana ilichukua mwendo gani wa tendo?

      19 Je! jamii ya Yohana, kikundi pekee duniani ambacho kilikubali kwa hamu nyingi Ufalme wa Kimesiya uliokuwa ukija, kilishiriki pamoja na Jumuiya ya Wakristo katika kumpa shikamoo huyo hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu? Mbali kabisa na hilo! Jumapili, Septemba 7, 1919, mkusanyiko wa watu wa Yehova kwenye Sida Pointi, Ohaiyo, ulikuwa na hotuba ya watu wote iliyokuwa na kichwa “Tumaini kwa Binadamu Wenye Kutaabika.” Siku iliyofuata, Star-Journal ya Sandusky iliripoti kwamba J. F. Rutherford, katika kuhutubia watu karibu 7,000, alikuwa “amesisitiza kwamba kutopendezwa kwa Bwana ni hakika kutajilia Ushirika . . . kwa sababu viongozi wa kidini—Wakatoliki na Waprotestanti—wakidai kuwa wawakilishi wa Mungu, wameacha mpango wake na wakakubali Ushirika wa Mataifa, wakiushangilia kuwa wonyesho wa kisiasa wa ufalme wa Kristo duniani.”

      20. Ni kwa sababu gani ilikuwa kufuru viongozi wa kidini kushangilia Ushirika wa Mataifa kuwa “wonyesho wa kisiasa wa Ufalme wa Mungu duniani”?

      20 Ushinde wenye kusikitisha sana wa Ushirika wa Mataifa ulipaswa kuashiria viongozi wa kidini kwamba vyombo hivyo vyenye kufanywa na mwanadamu si sehemu ya Ufalme wa Mungu duniani. Ni kufuru kama nini kudai hivyo! Hufanya ionekane kana kwamba Mungu alishiriki kufanyiza Ushirika wa Mataifa ambao ni kazi ya ovyo sana. Kwa habari ya Mungu “utendaji wake ni mkamilifu.” Ufalme wa Yehova wa kimbingu chini ya Kristo—wala si muungano wa wanasiasa wenye kuzozana, wengi wao wakiwa hawaitikadi kuwako kwa Mungu—ndiyo njia ambayo kwayo yeye ataleta amani na kufanya penzi lake lifanywe duniani kama katika mbingu.—Kumbukumbu 32:4; Mathayo 6:10, NW.

      21. Ni nini kinachoonyesha kwamba kahaba mkubwa anaunga mkono na kusifu mno mwandamizi wa Ushirika, Umoja wa Mataifa?

      21 Namna gani mwandamizi wa Ushirika, Umoja wa Mataifa? Tangu mwanzo wao, baraza hili limekuwa na kahaba akilipanda mgongoni mwalo, akishirikiana nalo waziwazi na akijaribu kuongoza liendako. Mathalani, katika ukumbusho wa mwaka wao wa 20 katika Juni 1965, wawakilishi wa Kanisa Katoliki la Roma na Kanisa Orthodoksi la Mashariki, pamoja na Waprotestanti, Wayahudi, Wahindu, Wabuddha, na Waislamu—waliosemekana kuwakilisha idadi ya watu wa dunia elfu mbili milioni—walikusanyika katika San Francisco kusherehekea uungaji-mkono na usifaji wao wa UM. Alipozuru UM Oktoba 1965, Papa Paul 6 alieleza habari zao kuwa “hilo tengenezo la kimataifa kubwa zaidi ya yote” na akaongeza: “Vikundi vya watu wa dunia vinategemea Umoja wa Mataifa kuwa ndilo tumaini la mwisho la itifaki na amani.” Mgeni mwingine wa kipapa, Papa John Paul 2, akihutubia UM katika Oktoba 1979, alisema: “Mimi natumaini Umoja wa Mataifa utadumu daima ukiwa ndilo baraza kuu la amani na haki.” Kwa uwazi sana, huyo papa alimtaja Yesu Kristo na Ufalme wa Mungu mara chache sana katika hotuba yake. Wakati wa ziara yake United States katika Septemba 1987, kama ilivyoripotiwa na The New York Times, “John Paul alisema kirefu juu ya daraka chanya la Umoja wa Mataifa katika kuendeleza . . . ‘ushirikiano mpya wa ulimwenguni pote.’”

  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • b Kitabu cha historia cha William L. Shirer The Rise and Fall of the Third Reich hutaarifu kwamba von Papen alikuwa “mwenye daraka zaidi ya mwingine yeyote katika Ujeremani la Hitla kupata mamlaka.” Katika Januari 1933 aliyekuwa chansela wa Ujeremani von Schleicher alikuwa amesema hivi juu ya von Papen: “Yeye alithibitika kuwa aina ya haini ambaye kando yake Yudasi Iskariote ni mtakatifu.”

  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Sanduku katika ukurasa wa 237]

      Churchill Afichua ‘Ukahaba’

      Katika kitabu chake The Gathering Storm (1948), Winston Churchill huripoti kwamba Hitla alimweka rasmi Franz von Papen kuwa waziri wa Ujeremani kwenye Vienna ili “kudhoofisha au kuvuta watu mashuhuri katika siasa za Austria.” Churchill hunukuu waziri wa U.S. katika Vienna kuwa akisema hivi juu ya von Papen: “Kwa jinsi ya ujasiri zaidi sana na ya kudharau zaidi sana . . . Papen aliendelea kuniambia kwamba . . . yeye alikusudia kutumia sifa yake akiwa Mkatoliki mwema apate uvutano pamoja na Waaustria kama Kardinali Innitzer.”

      Baada ya Austria kukubali ushinde na vikosi vya Hitla vyenye kushambulia ghafula vikiwa vimepiga gwaride kuingia Vienna, Innitzer kardinali Mkatoliki aliamuru kwamba makanisa yote ya Austria yapandishe bendera ya swastika, yapige kengele zayo, na yatoe sala kwa ajili ya Adolf Hitla kwa heshima ya ukumbusho wa siku ya kuzaliwa kwake.

  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 238]

      Chini ya kichwa hiki, makala inayofuata ilitokea katika chapa ya kwanza ya The New York Times ya Desemba 7, 1941:

      ‘SALA YA VITA’ KWA AJILI YA REICH

      Maaskofu wa Kikatoliki katika Fulda Waomba Baraka na Ushindi

      Kongamano la Maaskofu wa Kikatoliki wa Ujeremani lililokusanyika katika Fulda limependekeza ianzishwe ‘sala ya vita’ maalumu ambayo itasomwa mwanzoni na mwishoni mwa ibada zote za kimungu. Sala hiyo husihi Mungu abariki silaha za Ujeremani kwa ushindi na kutoa himaya kwa maisha na afya ya askari-jeshi wote. Maaskofu hao waliwaagiza zaidi makasisi wa Kikatoliki waweke na kukumbuka katika mahubiri maalumu ya Jumapili angalau mara moja kwa mwezi askari-jeshi Wajeremani ‘barani, baharini na hewani.’”

      Makala hii iliondolewa kwenye chapa za baadaye za nyusipepa hiyo. Desemba 7, 1941, ndiyo siku Japani, nchi fungamani na Ujeremani, iliposhambulia meli za U.S. kwenye Pearl Harbor.

      [Picha katika ukurasa wa 244]

      “Majina ya Kufuru”

      Hayawani-mwitu mwenye pembe mbili alipoendeleza Ushirika wa Mataifa baada ya Vita ya Ulimwengu 1, hawara zake wa kidini walitafuta mara hiyo kulipa tendo hilo idhini ya kidini. Kama tokeo, tengenezo jipya la amani ‘likajawa na majina ya kufuru.’

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki