Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 10/06 uku. 30
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—2006
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Wamefungwa Miaka 12 Gerezani?
  • Je, Intaneti Inahatarisha Wanyama pori?
  • Nishati Isiyoharibu Mazingira Yatumiwa Kupashia Nyumba Joto
  • Tambi za Miaka 4,000
  • Mafuta Yenye Thamani ya Mediterania
    Amkeni!—2008
  • Mzeituni Unaostawi Katika Nyumba ya Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Mafuta
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • Shangilia! Mashinikizo Yanafurika kwa Mafuta
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2006
g 10/06 uku. 30

Kuutazama Ulimwengu

◼ “Uhusiano uliopo kati ya jeuri inayoonyeshwa kwenye vyombo vya habari na jeuri miongoni mwa vijana ni mkubwa sana, karibu kama uhusiano uliopo kati ya uvutaji wa sigara na kansa ya mapafu.”—THE MEDICAL JOURNAL OF AUSTRALIA.

◼ Kuna uthibitisho unaodokeza kwamba “huenda virusi vya Ebola huishi na kusitawi ndani ya” popo wanaokula matunda, ambao huliwa katika maeneo fulani ya Afrika.—MACLEANS, KANADA.

◼ Takwimu za ofisi ya mkuu wa sheria huko Mexico zinaonyesha kwamba kwa zaidi ya miaka minane iliyopita, watoto wasiopungua 130,000 nchini humo wametekwa nyara ili wauzwe, watumiwe kingono, watumikishwe, au ili viungo vya miili yao vitolewe na kuuzwa.—MILENIO, MEXICO.

Kwa Nini Wamefungwa Miaka 12 Gerezani?

Mashahidi watatu wa Yehova wamefungwa huko Sawa, Eritrea, Afrika Mashariki, kwa miaka 12 iliyopita. Hawajafunguliwa mashtaka wala kufikishwa mahakamani. Wamezuiwa wasitembelewe na wageni, kutia ndani familia zao. Kwa nini? Kwa sababu hawataki kujiunga na jeshi. Sheria za Eritrea hazimruhusu mtu kukataa kufanya mambo fulani kwa sababu ya dhamiri. Vijana wanapokamatwa, wao huzuiliwa kwenye kambi ya kijeshi, ambako mara kwa mara wanapigwa na kuteswa kwa njia mbalimbali.

Je, Intaneti Inahatarisha Wanyama pori?

Gazeti The New York Times linauliza hivi: “Je, Intaneti inaharakisha kupungua kwa tembo wa Afrika?” Baadhi ya wanaharakati wa wanyama pori wanaamini inafanya hivyo na kwamba wanyama wengine wengi wamo hatarini pia. Kadiri idadi ya vituo vya Intaneti inavyoongezeka, ndivyo biashara haramu ya wanyama pori katika Intaneti inavyopanuka. Uchunguzi wa miezi mitatu uliohusu vituo vya Kiingereza uligundua kwamba, “zaidi ya bidhaa 6,000 za wanyama pori zilizo haramu au zinazoweza kuwa haramu zilikuwa zikiuzwa.” Bidhaa hizo zinatia ndani magamba ya kobe, sanamu zilizotengenezwa kwa mifupa ya tembo, na hata chui weusi walio hai.

Nishati Isiyoharibu Mazingira Yatumiwa Kupashia Nyumba Joto

Gazeti El País la Hispania linasema kwamba “sasa mbegu za zeituni zinatumiwa kutokeza nishati ya kupashia nyumba joto.” Chanzo hicho cha nishati kinatumiwa kupasha joto na kuchemsha maji kwenye nyumba 300 hivi huko Madrid. Mbegu za zeituni ni chanzo cha nishati cha gharama ya chini, kwani gharama yake ni ya chini kwa asilimia 60 inapolinganishwa na mafuta na asilimia 20 inapolinganishwa na makaa ya mawe. Hazichafui mazingira kwani kiwango cha kaboni dioksidi kinachotoka wakati zinapoungua ni sawa na kile kinachotoka zinapokuwa zikioza. Faida nyingine ni kwamba zinapatikana kwa urahisi. Zinapatikana baada ya mafuta kukamuliwa kwenye zeituni, na inasemekana Hispania ndiyo inayoongoza duniani kwa uzalishaji wa mafuta ya zeituni.

Tambi za Miaka 4,000

Gazeti The New York Times, linaripoti kwamba wanasayansi wanasema wamefukua zile wanazoziita “tambi za zamani zaidi duniani.” Tambi hizo zilikuwa nyembamba, zenye urefu wa sentimeta 50, na zilitengenezwa kutokana na mtama fulani wa China. Zilipatikana kwenye bakuli la udongo lililofunikwa, meta tatu chini ya ardhi karibu na Mto Huang kaskazini magharibi mwa China. Kulingana na jarida Nature, huenda eneo hilo liliharibiwa na tetemeko la ardhi na “mafuriko mabaya” yapata miaka 4,000 iliyopita. Kuhusu mjadala uliopo wa kama tambi zilianza kutengenezwa Italia, Mashariki ya Kati, au Nchi za Mashariki, gazeti Times linasema kwamba Houyuan Lu wa Taasisi ya Sayansi ya China, ambaye ni mmoja wa wagunduzi hao, anadai hivi: “Ugunduzi huu umethibitisha kwamba tambi za zamani zaidi zilitengenezewa China.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki